MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI
NA MAZINGIRA JIJINI TANGA,MHANDISI,JOSHUA MGEYEKWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA
HABARI
UHARIBIFU na Uchafuzi wa vyanzo vya mto zigi ambao
ndio chanzo pekee cha maji kwa jiji la Tanga kunakosababisha ujaaji tope kwenye
bwawa la maji na kupungua ubora wa maji ni miongoni mwa changamoto
zinazoikabili mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Tanga(Tanga
UWASA).
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa
Mamlaka hiyo,Mhandisi Joshua Mgeyekwa wakati akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu maadhimisho ya wiki ya Maji yatayoanza kesho mpaka Machi 22 mwaka uu
jijini Tanga.
Amesema ili kuweza kukabiliana na hilo mamlaka hiyo
ina kamati ya mazingira kuzunguka bwawa hilo kwa kushirikiana na WWF(T)
imeshaingia makubaliano na kikundi cha umoja wa wakulima wahifadhi mazingira
kuhihwi Zigi (UWAMAKIZI tangu Novemba mwaka jana kwa kipindi cha miaka
mitatu ili kukindi hicho kiweze kufanya hifadhi ya vyanzo vya mto zigi.
Katika maeneo ya vijiji vya Kimbo,Mashewa, Kwaisaka,
Shembekeza na Mashewa ambapo watu wapatao 374 wamejiunga na kikundi hicho
ambapo Tanga UWASA itachangia sh.milioni 100 kwa kikundi hicho katika kipindi
cha miaka mitatu.
Aidha amesema changamoto nyengine inayowakabili
ni utegemezi wa umeme wa TANESCO ambapo inatarajiwa hapo baadae kupitia “Water
Sector Development Program –WSDP huu ni mpango wa kuboresha miundombinu ya maji
unaofadhiliwa na benki ya dunia na serikali ya Tanzania
kutanunuliwa “Standby Generators ili pale penye katiko la umeme la muda mrefu
kuwashwe kupitia Generator hilo.
Akizungumzia mafanikio,Mhandisi Mgeyekwa amesema tokea
kuanzishwa mamlaka hiyo miaka kumi na tano iliyopita wamefanikiwa
kupunguza upotevu wa maji kutoka asilimia 45 hadi kufikia asilimia 23.4 kufikia
desemba mwaka jana.
Ikiwemo kuongeza eneo la utoaji huduma kwa wateja
kutoka asilimia 72 mwaka 1998 hadi kufikia asilimia 94.5 Juni mwaka jana pamoja
na kuongezeka kwa upatikanaji maji safi na salama kutoka wastani wa saa kumi na
nane hadi kufikia 23.5 kwa siku hadi February 2014.
Maadhimisho ya wiki ya maji mwaka huu yana kwenda
sambamba na kauli mbiu isemayo Uhakika wa maji na nishati ambapo maadhimisho
hayo yatakwenda samba na wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuunganisha maji kwa
wateja mbalimbali,mkutano wa wadau ikiwemo wenyeviti wa mitaa na
vitongoji vya Jiji la Tanga,Kupanda miche ya mkonge eneo la mamlaka utofu.
EmoticonEmoticon