MAGADI SODA KULIINGIZIA TAIFA SHILINGI BILIONI 480 KWA MWAKA
Meneja
Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel
Ngapemba akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi
wa Idara ya habari MAELEZO. Katikati ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya
Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga, na Mwisho ni Afisa Habari wa
Idara ya habari Frank Mvungi
Meneja
Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel
Ngapemba akifanunua kwa waandishi umuhimu wa mradi wa uchimbaji magadi
soda katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya
habari MAELEZO. Kushoto ni Mhandisi wa mradi Godfrey Mahundi na Kulia ni
mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga
Mhandisi
wa mradi wa magadi soda Godfrey Mahundi akitoa ufafanuzi kuhusu
makadirio ya gharama za mradi huo ambao unakadiriwa kutumia kiasi cha
dola za kimarekani milioni 500. Katikati ni Meneja Uhusiano na
Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba na wa
mwisho ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah
Mandwanga
PICHA ZOTE NA. Georgina Misama-MAELEZO
……………………………………………………………………..
Frank Mvungi-MAELEZO
IMEELEZWA
kuwa Tanzania ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa magadi soda
yatakayoingizia taifa Shilingi Bilioni 480 kwa mwaka.
Hayo
yamesemwa na Meneja Uhusiano na Mawsiliano wa Shirika la Taifa la
Maendeleo (NDC), Abel Ngapemba akizungumza kwenye mkutano na waandishi
wa habari leo jijini Dar es salaam.
Ngapemba
alisema hatua hiyo inatokana na kugunduliwa kwa kwa kiasi kikubwa cha
madini hayo katika Bonde la Engaruka Wilayani Monduli mkoani Arusha.
Alizitaja
faida za kugundulika kwa madini ya magadi soda kuwa ni ajira zaidi ya
500 na fedha za kigeni kutokana na mauzo ya madini hayo nje ya nchi.
Alisema
kuwa viwanda vinavyotegemea magadi soda kama malighafi ya uzalishaji
hali itakayochochea kukua kwa sekta ya viwanda hapa nchini.
Ngapemba
alibainisha kuwa madini ya magadi soda yanatumika viwandani katika
utengenezaji wa bidhaa kama vioo, sabuni, dawa za meno, dawa za
hosipitali, uoakaji mikate, kutengeneza karatasi, nguo, na usafishaji
wa maji.
Alifafanua
kuwa utafiti uliofanywa na wataalamu wazalendo kuanzia mwaka 2010 hadi
2013 na ulifanyika kwa awamu tatu yakwanza ikiwa ni uchunguzi wa awali
na kutafuta maeneo ya kufanyia uchorongaji ili kubaini wingi na ubora wa
magadi soda.
Alisema
kuwa kazi iliyofanywa na kampuni ya OC, ambapo awamu iliyofuata ni
kuangalia njia ya uvunaji wa magadi soda hayo iliyofanywa na JSC
Service.
“Matokeo
ya utafiti huo yameonyesha kuwapo kwa magadi soda kiasi cha mita za
ujazo bilioni 4.7 na inakadiriwa kila mwaka wastani wa mita za ujazo
milioni 1.9 zinaongezeka katika eneo hilo”, alisema Ngapemba na
kuongeza:
Alisema
kuwa NDC itahakikisha kuwa katika utekelezaji wa miradi hii mazingira
hayataathiriwa na tunu za taifa zitalindwa ambapo mtazamo wa shirika
hilo ni kuwapo kwa mradi wa uvunaji magadi, utalii, na ufugaji.
EmoticonEmoticon