Viongozi wa Barclays Africa Group walivyotembelea nchini
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Barclays Africa, Kennedy Bungane (kushoto)
akimsikiliza Balozi wa Malawi nchini, Bi. Flossie Asekanao
Gomile-Chidyaonga wakati wa mkutano uliondaliwa kwa wateja na wadau
wakati viongozi wakuu wa Kundi la Barclays Afrika (the Group),
wakitembelea nchini, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati
ni Ofisa Mkuu Vihatarishi (Risk) wa Barclays Afrika, Anil Hinduja.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Africa, Kennedy Bungane (kulia)
akisalimiana Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Chemi & Cotex,
Lakshmi Narayan wakati wa mkutano uliondaliwa kwa wateja na wadau
wakati viongozi wakuu wa Barclays Afrika, wakitembelea jijini Dar es
Salaam. Katikati ni baadhi ya maofisa wa NBC, Daniel Kaila (wa pili
kushoto) na Azza Ernest Mnzava. Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Barclays Africa, Kennedy Bungane (kushoto)
akibadilishana mawazo na Mkuu wa Huduma Rejareja za Kibenki wa NBC,
Mussa Jallow katika mkutano uliondaliwa kwa wateja na wadau wakati
viongozi wakuu wa Barclays Afrika, wakitembelea nchini.. Wengine kulia
ni Mkurugenzi wa Bodi ya NBC, Dr Hussein Kassim na Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Chemi & Cotex, Lakshmi Narayan. Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Bi. Mizinga Melu (kushoto) akiwa na
baadhi ya wageni waalikwa katika mkutano huo jijini Dar esd Salaam.
Ofisa
Mwendeshaji Mkuu wa NBC Tanzania, Maharage Chande (kulia), akisalimiana
na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Nyanza Mines, Mukesh Mamlani wakati
wa mkutano huo jijini Dar es Salaam. Katikati ni baadhi ya maofisa wa
NBC, Godfrey Nderingo (wa pili kushoto) na Cletus Shirima. Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kushoto) akiwa na wageni
wengine katika mkutano huo. Kundi la Barclays Afrika ‘the Group’,
limetokana na kuunganishwa kwa Kundi la ABSA ya Afrika Kusini (ABSA
Group Ltd) na sehemu kubwa ya shughuli za Benki ya Barclays barani
Afrika hapo Juni
31, 2013. ABSA (sasa the Group) ikimiliki asilimia 55 ya hisa ndani ya
NBC, serikali ya Tanzania asilimia 30 zinazobaki zikimilikiwa na
mashirika ya fedha ya kimataifa.
EmoticonEmoticon