CCM YASHINDA KWA KISHINDO KIKUU JIMBO LA KALENGA
Mbunge mteule wa jimbo la Kalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa
akibebwa juu na wanachama wa CCM huku wakiserebuka kusherekea ushindi
katika ofisi kuu ya CCM mkoa wa Iringa ambapo CCM imeshinda kwa mbali
katika matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika jana kwenye jimbo la
Kalenga mkoni Iringa, Tume ya taifa ya uchaguzi imemtangaza Godfrey
Mgimwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo ambapo CCM imeshinda kwa kura
22962 huku CHADEMA ikipata 5853 na chama cha CHAUSTA kura 150 Chama cha
Mapinduzi kimefanikiwa kushinda katika kata zote kumi na tatu za jimbo
hilo.
Watu wengi walijitokeza asubuhi kupiga kura na hali ilikuwa ni ya
utulivu kabisa na watu wengi waliopiga kura wameishukuru serikali na
tume ya uchaguzi kwa kuandaa utaratibu mzuri na kufanyika kwa uchaguzi
wenye utulivu..(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KAlENGA)
MATOKEO KAMILI HAYA HAPA
EmoticonEmoticon