February 04, 2014

HATIMAYE UVCCM MKOA WA MOROGORO WAMPA UVCCM FEKI ZA USO LEO LIVE!!

UVCCM Feki Apewa Za Uso!!

 Mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa Morogoro Harriet Sutta akiwa na katibu wake Nicodemas Tambo wakizungumiza juu matamko yanayotolewa na baadhi ya viongozi mkoani hapa kinyume na taratibu.
Mimi nazungumzia juu ya uchaguzi tulionao mbele yetu katika wilaya ya Gairo ludewa na Tungi Manispaa ya Morogoro, vijana washiriki kikamilifu kufanya kampeni za amani na utulivi na sio vurugu.





TAARIFA YA UVCCM MKOA WA MOROGORO KWA WAANDISHI WA HABARI.
Ndugu zangu waandishi wa habari Mliokusanyika Hapa ….
 
Kaka zangu na dada zangu asalamu alekum….
Tumsifu yesu kristo……………
 
Awali ya yote, kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema kwa kutukutanisha pamoja katika siku hii ya leo ili tupate kuongea machache yanayoendelea katika Taifa letu na husani katika chama chetu cha Mapinduzi CCM. Lakini Pia niwashukuru sana kwa kukubali kuitikia wito wangu na kufika mahala hapa kwa wakati na kwa mda muafaka Nawashukuruni sana, Na nawasahii muendelee na Moyo huo huo, mara zote mkihitajika sehemu yoyote ile, Maana ninyi ni nguzo Muhimu saana katika kuupa uma wa watanzania taarifa mbalimbali zinazoendelea katika Taifa lao.
 
Baada ya kusema hayo sina Budi kuwaelezeni sasa kwa nini Nimekuiteni hapa, Siku chache zilizopita mnamo Tarehe 2/02/2014 chama cha mapinduzi kiliazimisha Miaka 37 ya kuzaliwa kwake, sherehe hizo zilifanyika katika Mkoa wa Mbeya  na kuongozwa na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Taifa  na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwa Naiba Ya jumuiya ya Vijana wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro  (UVCCM ) ninachukua Nafasi hii Kumpokeza Mweshimiwa Dr. Jakaya Kikwete Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa kwa Hotuba yake nzuri alioitoa katika kilele hicho cha maadhimisho ya sherehe hizo za kuzaliwa kwa CCM. Lakini pia Kwa niaba ya UVCCM mkoa wa morogoro ninaomba yale yote alioyoyagiza Yatekelezwe Haraka kwani ninaamini yatafufua uhai wa chama na Kukiimarisha zaidi lakini pia kukiletea chama cha Mapinduzi Ushindi endapo yatatekelezwa  kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
 
Ndugu zangu waandishi wa habari, Lakini pia nichukue nafasi hii kurekebisha baadhi ya mambo yaliojitokeza katika Mkoa  wetu wa Morogoro Hasa katika Jumuiya yetu ya  Vijana. Kumekumekuwepo na Matamko mbalimbali yaliotolewa na baadhi ya  viongozi wa jumuiya  Yakihusishwa na Umoja wa Vijana Mkoa wa Morogoro. Naomba ifahamike kua uvccm ni taasisi ambayo ina miongozo na mfumo rasmi wa utekelezaji wa shughuli zake za kila siku.  Hivyo basi kwa mujibu wa kanuni za umoja wa vijana Msemaji wa Jumiya ya Vijana mkoa wa Morogoro Ni mwenyekiti wa UVCCM MKOA au Katibu Wa UVCCM Mkoa kama italazimika Mtu mwingine kusema basi ni kwa idhini maalumu ya Mwenyekiti
 
Wahenga walisema “kila panapotokea  kosa lolote lile  kuna jambo  la kujifunza” hivyo hakuna kosa lisilo na faida  Kupitia haya yaliotokea katika Mkoa wetu naomba pia iwe Fundisho kwenu waandishi  habari kila mkiitwa na Mtu yoyote anaetaka kuongea nanyi kama anaongea nanyi kwa niaba ya Tasisi ni vema mkafwatalia na mkajiridhisha kama ni Msemaji sahihi wa Tasisi Hiyo ili Kuepuka malumbano yasio na Tija
 
Kabla sijamaliza ningeomba pia kuchukua Fursa hii kuwapatia pole wakazi wa wilaya ya Kilosa kwa mafuriko yaliowapata ninaamini wapo katika wakati Mgumu hasa baada ya kuharibiwa makazi yao, na kuharibiwa mali zao. Nichukue nafasi hii kuwatia Moyo na kuwahakikishia serikali ya Chama cha Mapinduzi itahakikisha wanapatiwa stahiki zote anazotakiwa mtu kupewa na serikali yake yanapotokea majanga kama hayo.
 
Lakini pia niyaombe mashirika yasio ya kiserikali mashirika ya kimataifa na wadau mbalimbali wenye uwezo kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenda kuwafariji wana kilosa waliopatwa na mafuriko hayo na kuwaapa misaada ya kila namna inayostahili.
 
Mwisho ninaomba Kampeni zinazoendelea katika Mkoa wetu kata ya Tungi na Rudewa zifanyike kwa amani na ninawaomba vijana wa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo mdogo kua wastaarabu na waadilifu wajivunie kulinda misingi ya Taifa hili amani upendo na mshikamano uchaguzi usiwagawe na kueneza chuki baina yao hivyo ninawasihi washiriki kampeni hizo kwa amani na utulivu “wakubali kutofautiana kisera na kwa hoja ” ila “wasikubali kufarakana” Vijana tunahitaji Uvumilivu wa kisiasa ili tukomae katika siasa na Demokrasia ya kweli
 
Niwashukuru saana kwa Kunisikiliza…..
Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa
 
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na Harriet Sutta
MWENYEKITI WA UVCCM MKOA
MOROGORO
04/01/2014

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »