February 04, 2014

LIVEEE,MH:MWIGULU NCHEMBA ANASA WATOROSHAJI WA BIDHAA MPAKANI MWA -TANZANIA NA MALAWI

Naibu Waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na Naibu Kamishina Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa Tanzania,Ndugu Patric Kisaka(kulia) na Mkurugenzi wa huduma za Ulipaji Kodi na Elimu Ndugu,Richard Kayombo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Bi.Magreth Kalenga(hayupo pichani) wakiondoka kwenye Ofisi za TRA Kuelekea kwenye eneo la Mpakani Mwa-Tanzania na Mawali wilayani Kyela hii leo.
 Kibao Kianachoonesha "KARIBU TANZANIA" kilichopo pembezoni mwa Mto Songwe unaotumiaka kama mpaka wa Tanzania na Malawi.
Huu ndio Mto Songwe ambao ni Mpaka wa Tanzania na Malawi Wilayani Kyela.Huu mto umeleelekea hadi Ziwa Nyasa na ndio Mpaka wa Tanzania na Malawi,Lakini sehemu kubwa ya Mto huu kunavipenyo visivyo rasmi vinavyotumika na Wananchi Kuvusha Biashara za Magendo na Kukwepa kulipa kodi kwa kupita kwenye Kivuko rasmi cha Kasumulu hapa Kyela.
 
 Msafara wa Naibu Waziri wa Fedha umefika kwenye hiki Kipenyo cha Mto Songwe(Kinajulikana kama Timotheo) kinachotumika na Wananchi wasio wazalendo Kuvusha bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania -Malawi au Malawi kuja Tanzania.Ng'ambo ya Mto unaonekana ni mzigo mkubwa wa sukari unaotarajiwa Kuvushwa kuja Tanzania kwa njia za Magendo na kubwa zaidi Kukwepa Ulipaji Kodi.
Naibu Waziri wa Fedha akiangalia Moja ya Mtumbi unaotumiaka kuvushia Biashara za Magendo kwenye hiki kivuko haramu cha Timotheo kwenye Mto Songwe.
 Naibu Waziri na Msafara wake wakiwa kwenye Kivuko Kingine kisicho rasmi kinachotumika Kuvushia bidhaa za magendo kutoka Nchi hizi mbili za Tanzania na Malawi.Ng'ambo kwenye Nyumba zinazoonekana ni Nyumba za Wananchi wa Malawi.Na kwa mbali kunaonekana roli likiwa limepakia Mzigo unaodaiwa kuwa ni Mpunga uliovushwa kwa Magendo kutoka Tanzania kwenda Malawi.
Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba akifanya mahojiano na Vijana waliokutwa wakivusha sukari kutoka Malawi kuja Tanzania.Vijana hao wanadai wanalazimika kutumia njia hizi haramu kuvusha Sukari kutokana na kuwa na mitaji midogo ya biashara zao,Hivyo kupita kwenye Kivuko Rasmi cha Kasumulu wanakatwa Kodi Kubwa ambayo inawafanya wakose faida kwenye Biashara yao.
Naibu Waziri wa Fedha akizungumza na Watumishi/Watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Watumishi wa Idara mbalimbali zinazohusika na Mpaka wa Tanzania na Malawi.
Na.Habari Kwanza Blog,
Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Lameck Nchemba hii leo(Tar.04/02/2014) ameendelea na Ziara yake ya Kikazi Mkoani Mbeya ya Kutembelea Vituo vya Ukusanyaji wa Mapato na Kuangalia changamoto za Ukusanyaji wa mapato kwenye maeneo ya Mipaka ya Nchi.
Hii leo amefika Wilaya ya Kyela na kukutana na Mkuu wa Wilaya Mh:Magreth Kalenga aliyeongoza kutembelea maeneo ya Mpaka wa Tanzania na Mawali kutathimini namna Ukusanyaji wa Mapato unavyokuwa na changamoto nyingi kutokana na Watanzania wengi kukwepa Kulipa kodi kwenye Vivuko rasmi vya Mipaka.
Wilaya ya Kyela imetajwa kuwa na Vipenyo visivyo rasmi 32 vinavyotumika kupitisha bidhaa za magendo(sukari, Viroba,Mpunga n.k) ,Katika hali ya kuonesha kuwa biashara ya Magendo imeshamili mpakani hapo,Naibu Waziri wa Fedha ameshuhudia vijana wakivusha Sukari kutoka Malawi kuja Tanzania kwenye kipenyo kisicho rasmi kinachojulikana kwa jina la Timotheo.Katika mahojiano ya Mh;Mwigulu na Vijana hao,Watanznaia hao wanasema walazimika kutumia njia hizo za panya kuvusha bidhaa hizo kwasababu ya Ushuru kuwa Mkubwa na Mtaji wao ni mdogo,pia Ugumu wa Maisha ndio unawafanya wakimbilie kutafuta faida ya haraka ilikusaidia familia zao.
Naibu Waziri amesema Kupitia Wizara yake(Serikali) imejipanga kufanikisha haya.
1.Kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa(Sukari n.k) nchini unaongezeka  ilikutoa nafasi ya wafanyabiashara kuchana na biashara za magendo za kutumia bidhaa za Malawi kwa njia ya kukwepa kodi.
2.Kuongeza Watumishi wa Kwenye Mipaka wanaohusika na Usalama,Ukusanyaji wa Mapato n.k ilikuhakikisha huduma zinatolewa kwa wakati bila usumbufu wowote.
3.Pia Ujenzi wa kituo kituo cha Pamoja(One-Stop Border Post) cha Ukaguzi kati ya Nchi ya Tanzania na Malawi ilikuondoa Urasimu na Ucheleweshwaji wa kupitisha bidhaa kwenye vivuko vya Mipakani.Mazungumzo yameshaanza na Utekelezaji unategemea kuanza mapema.
3.Kuongeza Upatikanaji wa Elimu kwa Wafanyabiashara kuhusu athari za kukwepa kodi,faida za kutumia Vivuko rasmi kwenye upitishaji wa bidhaa zao.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »