Na Boniface Wambura,Dar es Salaam.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesitisha matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye
viwanja vyote vyenye huduma hiyo ili kutoa fursa ya kufanyika tathmini ya kina
kabla ya kuendelea tena.
Uamuzi
huo umefikiwa kwa kuzingatia sababu mbalimbali baada ya kikao kati ya
Sekretarieti ya TFF na maofisa wa benki ya CRDB kilichofanyika jana (Februari 3
mwaka huu) katika ofisi za Shirikisho.
Tathmini
hiyo inafanyika ili kubaini changamoto zilizojitokeza na kuzitafutia ufumbuzi
kabla ya kuendelea tena na matumizi hayo, kubwa ikiwa ni hadhari iliyotolewa na
vyombo vya Usalama juu ya misongamano inayotokea uwanjani kutokana na
kutokuwepo mtiririko mzuri wa uingiaji.