February 04, 2014

HANDENI KUTUMIA ZAIDI YA TSH BIL. 7 KWA MWAKA 2014/15

{Mkurugenzi  Mji wa  Handeni    Thomas Mzinga  pichani}
                                                                    Raisa  Said, Handeni


Baraza la Halmashauri Mji wa Handeni limepanga kutumia jumla ya Sh. Bilioni 7.92 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo na utawala kwa mwaka wa fedha 2014/2015.

Kwa mujibu wa mapendekezo ya bajeti yaliyopitishwa na kikao cha Baraza la Halmashauri hiyo, kati ya fedha hizo Sh. milioni.503.19 zimepangwa kutuimika kwa ajili kutekeleza miradi mbalimbali za maendeleo kwa mwaka huo wa fedha.

Akisoma mapendekezo hayo katika kikao hicho kilichofanyika makao makuu ya Halmashauri hiyo, Chanika, Handeni , Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri,Thomas Mzinga alisema vyanzo vikuu vya fedha za utekelezaji wa miradi ni ruzuku kutoka serikali kuu na wahisani.



Mzinga  alisema  bajeti ya  mwaka  2014/2015 imeandaliwa  kufuatiwa  malengo makuu  saba  ambayo ni  Huduma  ya  ukimwi  kuboreshwa na  maambukizi  mapya  kupunguzwa ,  kuboresha upatikanaji wa  huduma za  jamii,  kuimarisha  shudghuli za  utawala  bora pamoja  kuboresha udhibiti wa  majanga.
Mingine ni miradi ya  kuimarisha  huduma  za  kijamii jinsia  na  kujenga  uwezo  wa  jamii na  kuongeza  idadi  na ubora  wa huduma  za  jamii na  miundombinu .


Mkurugenzi huyo  alisema  kuwa  mbali ya fedha  hizo  pia  wanapeleka  maombi  maalum  nje  ya  ukomo  wa  bajeti  yenye  thamani  ya  Tshs. 2,374,000,000 kati ya  hizo  mil.1.5  zitatumika  katika  kujenga  jengo  la  utawala  na  mil. 624,000,00/= zitatumika  katika  kujenga vyumba 13 vya  maabara pamoja  na  mil. 250,000,000/= zitatumika  katika  kununua  gari  la  Mkurugenzi  na  gari  la Idara  ya  mipango  .
Akizungumzia juu ya changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa  bajeti ya  2013/2014 ,
 alisema kuwa kuchelewa kwa fedha za  matumizi ya  kawaida  kutoka  serikali kuu (Hazina).

Alitaja chanhamoto nyingine kuwa ni kutopata fedha  za  maendeleo  kwa  wakati  kutoka  hazina (fedha  hizi  zinapitia Halmashauri  ya  wilaya  zinapotumwa

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »