WAMILIKI WA UWANJA WA MKWAKWANI KULA SAHANI MOJA NA TFF.

February 01, 2014
Na Oscar Assenga,Tanga.
WAMILIKI wa uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga wamesema kuwa endapo mapato yatakayotangazwa na bodi ya
ligi kuu kati ya Coastal Union na Yanga yatakuwa chini ya milioni 70 hawataridhika nao badala yake watazungumza na shirikisho la soka nchini TFF kuwaambia wauondoe mfumo kielectroniki kwenye uwanja huo kwa sababu utakuwa hauna manufaa kwao.

Kauli hiyo ilitolewa na TANGA RAHA BLOG Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(CCM)Gustav Mubba aliyema hayo jana wakati akizungumzia madhara yaliyotokana na mfumo huo ambao ulianza kutumika kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara akisema madhara mengine ni ununuzi wa tiketi kwenye vituo kuleta usumbufu kwa mashabiki wa soka kutokana na kununu lakini wakati wa utumiaji mfumo unakuwa taratibu wakati mwengine kugoma.

Mubba alisema utaratibu huu unawanyima  mapato wamiliki wa viwanja kwa sababu mpaka muda huu hawajui zimepatikana kiasia gani pamoja na kutokuwa na mwakilishi kwenye mchakato wa kusehabu mapato yaliyopatikana.


Aidha alilitaka shirikisho la soka hapa nchini TFF kuhairisha mfumo huo mpaka hapo watakapojipanga kwani adhari zake zimekuwa na kubwa sana licha ya kupoteza mapato lakini usalama wa mashabiki wa soka kuingia kwenye viwanja ni mdogo sana.

  "Nasema sisi kama walimiki wa uwanja wa Mkwakwani tunasema endapo mapato yatakuwa pungufu na mapato yaliyopatikana kwenye mechi ya Yanga na Coastal Union msimu uliopita tutauondoka mfumo huu kwa sababu utakuwa hauna manufaa kwetu "Alisema Mubba.

Mubba alisema kwa utaratibu huo wao kama wamiliki wa uwanja huo mpaka wakati huu wameshindwa kuelewa kiasi cha mapato kilichopatikana kwenye mechi hiyo hivyo mapato yatakayokuwa chini ya kiwango walichikitaja hapo juu wataelewa .

Hata hivyo Katibu Mubba alishangazwa na shirikisho la soka hapa nchini kwa kushindwa kuufanyia majaribio kwenye uwanja wa Taifa ili waweze kujua athari zake kabla ya kuuleta kwenye viwanja vya mikoani.

Alieleza mkataba wa kuuweka mfumo huo ulifikiwa na TFF na CRDB wakati wamiliki wa viwanja hawakushirikishwa zaidi ya kuambiwa mfumo huo utafungwa kwenye viwanja vyao.

  .....Leo ni siku ya tano wamiliki wa uwanja hawajajua mapato yaliyopatikana kwenye mechi hiyo na hawajui ni lini watajua na kwenye mchakato wa kuhesabu hawana mwakilishi hivyo hawajui nini la kufanya ......Alisema Mubba.

Kwa upande wake,Meneja wa Uwanja wa Mkwakwani,Mbwana Msumari alisema athari za mfumo huo zilianza kuonekana baada ya mashabiki wa soka kuvunja geti na kuingia uwanjani hapo kitendo ambacho kilileta hasara kwa wapenzi wa soka kuingia uwanja hapo bila kulipa fedha.

Msumari alisema athari nyengine ni mashabiki wa soka wanapokwenda uwanjani kuangalia mpira wanaambiwa mfumo umegoma kitendo ambacho kilipelekea mashabiki kupandwa na hasira na kulivunja geti na kuingia ndani.

Alisema kutokana na hilo tiketi za elifu 15,000 zilikuwa zinauzwa kwa sh,10,000 na zile za elfu 5000 zilikuwa zikiuzwa 2000 na mashabiki waliovunja geti na kubahatika kuingia uwanjani wakiwa na tiketi zao kutokana na kuvunja geti.

   "Naishauri bodi ya ligi wajipanga upya kuhusiana na mfumo huo yenye kama meneja wa uwanja hakufurahishwa na kitendo hicho hivyo bi bora mfumo huo usimame "Alisema Msumari.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »