*MWENYEKITI WA CCM DR. JAKAYA KIKWETE AWASILI MKOANI MBEYA KUHUDHURIA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM
Mwenyekiti
wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano akipunga mkono wakati
akishuka kutoka kwenye ndege jana jioni ya leo kwenye uwanja wa Kimataifa wa
Songwe mkoani Mbeya tayari kwa sherehe za kuzaliwa kwa CCM
zitakazofanyika tarehe 2 Februari ambapo asubuhi kutakuwa na matembezi
ya mshikamano kisha kuhitimishwa kwenye uwanja wa wa Sokoine.
Mwenyekiti
wa CCM Taifa,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho
Kikwete akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Phillip
Mangula mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Songwe tayari kwa maadhimisho ya sherehe za miaka 37ya kuzaliwa Chama
Cha Mapinduzi.
Mwenyekiti
wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wazazi Tanzania Ndugu Abdallaha Bulembo mara baada ya
kuwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya tayari kwa
sherehe za kutimiza miaka 37 tangia kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.
Mwenyekiti
wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya
Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbeya Mjini
Ndugu Ephraim Mwaitenda kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe
mkoani Mbeya.
Boda
Boda zikiongoza msafara wa Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete aliyewasili mkoani Mbeya
kwa ajili ya sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.
Bodaboda
zikiongoza msafara wa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete kutoka kwenye uwanja wa kimataifa
wa Songwe.
Mwenyekiti
wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya
Kikwete(katikati) akiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM mkoa wa Mbeya
tayari kuongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya mkoa wa Mbeya.
EmoticonEmoticon