February 01, 2014

JAJI MARK BOMANI ATETEA SERIKALI TATU

Dar es Salaam. Jaji mstaafu, Mark Bomani, ametetea kuwepo kwa muundo wa Serikali tatu na kuwabeza wanaodai kuwa ni wa gharama kubwa.
Amesema dhana hiyo si sahihi na kwamba anayedai kuwa itakuwa hivyo. Ni vyema akawa na ushahidi wa kina badala ya maneno matupu.
Kulingana na mapendekeo ya Jaji huyo kuhusu mabadiliko ya Katiba, ambayo Mwananchi ina nakala yake, suala la gharama kubwa za uendeshaji wa Serikali tatu halina msingi wowote.
“Naungana na Jaji Warioba hoja kwamba Serikali tatu ni gharama kubwa haina ushahidi wowote. Serikali tatu si lazima ziwe na gharama kubwa kuliko Serikali mbili na suala hilo linategemea mambo mengi,” alisema.
Alisema mathalan Bunge la sasa la Serikali mbili lina gharama kubwa kwa sababu lina wabunge 380 wakati Bunge la Muungano litakuwa na wabunge 75 na hata kama zikiongezeka gharama za Bunge jipya la Tanganyika bado kutakuwa na idadi ndogo ya wabunge.
“Hiyo inaashiria kuwa gharama za za kuendesha Bunge la Muungano na lile la Tanganyika zitapungua” alisema. Bomani alisema mfumo wa Serikali mbili una matatizo kwani hata Uingereza ambako kuna Serikali za idadi hiyo ikiwemo ya Ireland ya Kaskazini, kuna matatizo mengi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »