January 23, 2014

HALMASHAURI YA SIHA IMEPITISHA BAJETI YA SH. BILIONI 19.3

Na Omary Mlekwa, Siha

HALMASHAURI ya wilaya Siha mkoani Kilimanjaro imesema imeshindwa kukamilisha  kwa miradi ya kimaendeleo kwa wakati kutokana na kuchelewa kupokea fedha za miradi kutoka hazina  pamoja na uchache wa vyanzo vya mapato ya ndani pamoja na mabadiliko ya tabia nchini.

Akizungumza katika kikao maalumu  cha baraza la madiwani kujadili bajeti ya mwaka wa fedha wa 2014/2015, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Rashidi Kitambulio alisema uchelewashaji umesababisha miradi ya kielimu, afya miundombinu kukwama. Mkurugenzi huyo alisema mabadiliko ya tabia nchi yameathiri uzalishaji   wa mazao na kuathiri mapato yatokanayo na mazao mashambani ambapo kwa mwaka wa fedha 2012/2013 walikusudiwa kukusanya kiasi milioni 239,500,000 badala yake walishindwa kufikia lengo hilo.

Awali akitoa taarifa ya rasmi ya bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka fedha 2014/2015 mkurugenzi wa huyo alisema kuwa wanatazamia kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi bilioni 19.320,034,512 kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo ruzuku toka serikali kuu na mapato ya ndani.


Kitambulio alifafanua kuwa kiasi hicho  ni sawa na ongezeko la shilingi bilioni 2,297,943,008 ikilinganishwa fedha  zilizoidhinishwa katika  bajeti ya shilingi bilioni 17,022,091,594 ya mwaka wa fedha 2012/2013



Alisema katika bajeti hiyo wanakusudia kukusanya shilingi bilioni 1, 935,247,550kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani  ikiwemo ushuru wa masoko, ushuru wa vituo vya mabasi , ushuru wa mazao na vyanzo vingine vilivyopo katika halmashauri hiyo.


“Ndugu wa baraza la madiwani tunatazamia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 12,421,114,116 kwa ajili ya mishahara, miradi ya maendeleo shilingi bilioni 4,535,083,755, na matumizi ya kawaida shilingi bilioni 1,856,866,786,”alisema
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Siha, Rashid Kitambulio, akisoma mapendekezo katika Bajeti ya Halmashauri hiyo leo
“Na katika kuendeleza vijana na wanawake kupitia asilimia tano kwa kila kundi  rasmu hiyo ya bajeti tumetenga kiasi cha shilingi milioni 168,782,675 kutokana na mapato ya ndani nah ii ikiwa ni asilimia kumi ya mapato yote ya ndani na pia tumetenga kiasi cha shilingi milioni 337,565,510”alisisitiza Kitambulio
Sehemu ya Madiwani wakijadili Bajeti ya mwaka 2014/2015 katika kikao kilichofanyika leo, katika ukumbi wa Halmashauri
Hata hivyo wajumbe wa baraza hilo la madiwani walipitisha bajeti ya mapato na matumizi  kwa ajili ya halmashauri hiyo ya jumla ya shilingi bilioni 19.320,034,512.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »