DC SIHA AWATAKA WATAALAMU WA HALMASHAUTI KUIMARISHA UKUSANYAJI WA USHURU.

January 23, 2014
Na Omary Mlekwa,Hai.MKUU wa wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Dkt Charles Mlingwa amewataka wataalumu wa halamashauri hiyo kuimarisha hali ya ukusanyaji wa ushuru wa aina  mbalimbali bila kubugudhi wananchi ili kuongeza mapato ya ndani

Pia aliwataka wataalamu hao kuwa na  takwimu sahihi za walapi kodi
wakubwa na wadogo ili kuweza kuweka makisio ya mapato na matumizi yanayoendana na utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo

Akizungumza na wajumbe wa baraza pamoja na wananchi waliohudhuria
kikao maalumu cha baraza la madiwani cha kujadili na kupisha bajeti ya mwaka wa fedha wa mwaka 2014/2015 alisema wataalamu wakiimarisha ukusanyaji itasaidia kupunguza utegemezi  wa kutoka serikalini

Kauli hiyo aliitoa baada ya baadhi ya madiwani kupinga bajeti ya

ushuru wa mazao kwa madai kuwa inawaumiza wakulima wa mazao mbalimbali


Akitoa hoja hiyo diwani wa viti maalumu Claudi Muro  alisema suala
ushuru wa mazao katika masoko mengi limekuwa kero ambapo alitaka kujua serikali ya wilaya ina mpango gain wa kuondoka tatizo hilo?

Alisema  ushuru unatoza katika masoko unawaumiza wakulima na

kuwanufaisha wazabuni huku halmashauri ikiendelea kupoteza mapato kutokana na wakulima wengi kukwepa ushuru huo

Nae diwani wa kata ya Sanya Mjini Juma Jane alisema ushuru unaotozwa
na wazabuni ni kati ya shilingi 2500 hadi 4500  jambo ambalo limekuwa kero kwa wakulima na baadhi yao wamekuwa wakitafuta hata njia za panya ili kukwepa ushuru huo,

Alisema ushuru unatozwa katika halmashauri ya Siha ni mkubwa

ikilinganishwa na halmashauri za jirani ambapo halmashauri zote
zinazopakana  nazo zinatoza ushuru kati ya shilingi 500 hadi shilingi
1000

Akichangia hoja hiyo, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Jonathani

Nassari aliwataka wataalamu kuliangalia suala hilo kwa kina na kukaa na wazabuni ili kuweza kulitafutia ufumbuzi wa suala hilo

Akizungumzia hali hiyo  Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya hiyo
Rashid Kitambulio  mbali na kukiri kupokea malalamiko mengi juu ya tozo hizo alisema kuwa ofisi yake ina andaa utaratibu wa kukutana na wazabuni wote ili kuweza kuliangalia suala hilo kwa upya ikiwa ni juhudi za kuondoa kero hiyo.
 

Alisema katika maelekezo ya awali mzabuni huyo alielekezwa kukusanya kiwango kisicho zidi asilimiaa 5% kutoka kwa wafanyabishara hao wa mazao ya Chakula na kwamba mkataba huo pia uliwaondoa katika tozo hiyo wakulima wanaorudisha mazao yao kutoka shambani baada ya kuyavuna.


Awali akitoa taarifa ya rasmi ya bajeti ya makadirio ya mapato na

matumizi kwa mwaka fedha 2014/2015 mkurugenzi wa halmashauri Rashidi Kitambulio alisema kuwa wanatazamia kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi bilioni 19.320,034,512 kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo ruzuku toka serikali kuu na mapato ya ndani

Kitambulio alifafanua kuwa kiasi hicho  ni sawa na ongezeko la

shilingi bilioni 2,297,943,008 ikilinganishwa fedha  zilizoidhinishwa
katika  bajeti ya shilingi bilioni 17,022,091,594 ya mwaka wa fedha
2012/2013

Alisema katika bajeti hiyo wanakusudia kukusanya shilingi bilioni 1,
935,247,550kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani  ikiwemo ushuru wa masoko, ushuru wa vituo vya mabasi , ushuru wa mazao na vyanzo vingine vilivyopo katika halmashauri hiyo.

“Ndugu wa baraza la madiwani tunatazamia kutumia kiasi cha shilingi
  bilioni 12,421,114,116 kwa ajili ya mishahara, miradi ya maendeleo shilingi bilioni 4,535,083,755, na matumizi ya kawaida shilingi bilioni 1,856,866,786,”alisema

“Na katika kuendeleza vijana na wanawake kupitia asilimia tano kwa
kila kundi  rasmu hiyo ya bajeti tumetenga kiasi cha shilingi milioni 168,782,675 kutokana na mapato ya ndani nah ii ikiwa ni asilimia kumi ya mapato yote ya ndani na pia tumetenga kiasi cha shilingi milioni 337,565,510”alisisitiza Kitambulio
 Hata hivyo wajumbe wa baraza hilo la madiwani walipisha rasimu ya bajeti ya mapato na matumizi  kwa ajili ya halmashauri hiyo ya
shilingi  jumla ya shilingi bilioni 19.320,034,512

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »