KINGWENDU KUPAGAWISHA KWENYE BONANZA LA MICHEZO JUMAMOSI TANGA.

January 20, 2014
Na Burhan Yakubu,Tanga.

Msanii marufu wa sanaa za maigizo na uchekeshaji ,Kingwendu

anatarajiwa kushiriki katika bonanza litakalofanyika uwanja wa shule ya msingi majani mapana Jijini Tanga jumamosi ijayo januaria 25 mwaka huu.

Kingwendu atakuwa msanii mkaribishwa katika bonanza hilo ambalo
limekuwa likifanyika kila jumamosi ikiwa ni utekelezaji wa kamati ya uratibuinyaoongozwa na diwani wa kata ya Nguvumali,Mustapha Selebos iliyopanga kuwa itakuwa ikiwaalika wasanii na wachezaji mbalimbali kutoa burudani mjini Tanga.


Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika bonanza juzi jumamosi,
mjumbe wa kamati ya uratibu,Hamis Tembo alisema mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Halima Dendego.

Katika bonanza la juzi kundi la madansa kutoka Kigamboni Jijini Dar es
  salaam lijulikanalo “Best Love” liliweza kushangiliwa na mashabiki waliofurika katika uwanja huo na kuleta upinzani mkubwa kwa madansa waTanga.

Mbali ya kundi hilo la Kigamboni Dar es salaam,dansa mwenye umri mdogo
Mahfudh Ramadhani(6) alishangiliwa kutokana na kwenda sambamba na kundi la Hot Pot huku D.Doctor akiwakumbusha mashabiki wa Tanga nyimbo zake za zamani.

Kwa upande wa mpira wa miguu,timu ya Kagera FC iliifunga Jogoo bao
2-0,Masiwani Vijana ikatoka sare ya bao 1-1 na Chumbageni Veterani huku  Mapana ikitoka na ushindi wa bao bao 1-0 didi ya Police Jamii.

Netiboli zilicheza kwa kupokezana timu za Nguvumali,Mwamboni na
Vascodagama huku mpira wa Volleyboli zikicheza Eagle na Kai Star.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »