KISAUJI AWAFUNDA WANACHAMA WA CCM TAWI LA CHUO KIKUU ECKENFORDE TANGA.

January 20, 2014
Na Safari Chuwa ,Tanga.
VIJANA mkoani Tanga wametakiwa kusimama imara ikiwemo kuthubutu kujituma na kubuni ajira ambazo zitawawezesha kuyaendesha maisha yao badala ya kuendelea kukaa na kusubiria ajira ambazo huchukua muda mrefu kupatikana.

Ushauri huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na Mjumbe wa Halmashauri Kuu
  ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tanga (MNEC) Salim Kisauji wakati wa sherehe za ufunguzi wa tawi jipya la chama hicho lililopo kwenye chuo kikuu cha Eckenforde mkoani Tanga.


Kisauji alisema vijana wengi wamejijengea tabia ya kuacha kufanya kazi
wakifikiria maisha bora yanaweza kupatikana bila wao kuwajibika na kuwataka kubadilika kwa kuacha kuwa wategemezi kwenye jamii zao .     "Ipo tabia ya vijana wengi kuacha kufanya kazi na kutumia muda
mwingi kukaa vijweni hilo sio jambo nzuri lazima mbadilike kwa kubuni ajira mbadala zikazowawezesha kuendesha maisha yenu na jamii zenu husika "Alisma Kisauji.

Aidha aliwataka wanachama wa tawi hilo kuhakikisha wanakuwa mstari wa
mbele kukitetea chama hicho na kudumisha mshikamano ambao utawaletea maendeleo wao katika maisha yao ya sasa na baadae.

Katika ufunguzi huo,Kisauji alipokea wanachama wapya wa tawi hilo
wapatao 148 ambao aliwakabidhi kadi na kuwataka kutokubali kuyumbishwa badala yake kuwa imara kukitetea chama hicho ndani na nje

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chama cha
Mapinduzi (UVCC) wilaya ya Tanga,Salim Perembo aliwataka vijana kuacha kujisahau  hasa wakishapata elimu kwa kuwadharau wazazi na kuwaona hawana maana kwani kufanya hivyo itapelekea wao kushindwa kufikia malengo yao waliojiwekea.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »