UVCCM TANGA YAWATANGAZIA KIAMA MADIWANI,WENYEVITI MIZIGO.

January 20, 2014
Na Oscar Assenga, Kilindi.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga(UVCCM)Abdi Makange amewataka madiwani na wenyeviti wa serikali za vijiji na vitongoji wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo kwa wananchi kuacha kuchukua fomu za kugombea nafasi hizo katika uchaguzi mkuu ujao 2015.

Makange alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika mkutano wa hadhara uliofanyika
katika kijiji cha cha Makasia Kata ya Kwediboma wilayani hapa ambapo alisema viongozi wengi baada ya kupata nafasi za uongozi wamejisahau na kushindwa kutatua kero zinazo wakabili wananchi wao waliowachangua kitendo ambacho kinapelekea wananchi kuichukia serikali.


Alisema katika maeneo mbalimbali mkoani hapa viongozi hao wamekuwa
wakichangia kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi wao ikiwemo kusababisha migogoro baina ya wakulima na wafungaji kwa kugawa maeneo kwa wageni na kuwaacha wazawa wakiwa hawana ardhi kutokana na maslahi binafasi.     “Wenyeviti ambao wanachangia migogoro kwenye maeneo yao kiama chenu kinakuja nawaambiane  hatutafumbiwa macho ni lazima waondoke wapishe wengine wenye uwezo wa kuwafanya wananchi kuishi kwa amani na kutatua kero zao “Alisema Makange.

Mwenyekiti huyo alienda mbali sana kwa kusema kuwa viongozi wa aina
  hiyo hawafai kuwaongoza wananchi hivyo kuwataka wakamatwe na kuwekwa ndani kisha wafukuzwe katika maeneo yao.

Akizungumzia suala la mikopo asilimia 10 ya vijana na wakina mama
  inayotoka serikali kuu kwa ajili ya maendeleo yao inayokana na makusanyo ya Halmashauri alisema suala hilo sio ombi bali ni lazima hivyo maafisa wanahusika wahakikishe wanalipa msukumu mkubwa ili ipatikane kwa wakati.

Aliwataka vijana na wakina mama kuunda vikundi katika maeneo yao na
  kufuata taratibu zote zinazopaswa ili waweze kupata mikopo hiyo ambayo itaweza kuwakwamua kimaendeleo na kuchangia ongozeko la pato lao.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »