March 08, 2014

WAFANYAKAZI WANAWAKE KUTOKA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WAUNGANA NA WANAWAKE WENZAO KATIKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA WANAWAKE DUNIANI KATIKA UWANJA WA MWEMBE YANGA

 Wafanyakazi Wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiungana na wanawake wenzao kusherehekea siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 8, 2014.
 Baadhi ya wafanyakazi wanawake kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF wakiwa katika maandamano yaliyokuwa yakielekea katika Uwanja wa Mwembe Yanga Mapema leo Katika Kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani ambapo wafanyakazi wanawake wa PPF nao waliweza kujumuika na wanawake wenzao katika kusherehekea Siku hiyo
Wafanyakazi wa PPF wakiingia katika Uwanja wa Mwembe Yanga huku wakiwa na Bango lao linalosomeka "Chochea Mabadiliko Kuleta Usawa wa Kijinsia, PPF Fao la Elimu - Linazingatia Usawa wa Kijinsia"
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF (Waliovalia Fulana za Rangi ya Blue) wakiwa wameketi kwenye eneo lao huku wakifuatilia matangazo yaliyokuwa yakitolewa katika Uwanja wa Mwembe Yanga wakati wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Mwanamke Dunia.
Baadhi ya Wafanyakazi wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya Sherehe ya Sikukuu ya Wanawake Duniani ambayo imefanyika katika Uwanja Wa Mwembe Yanga, Wilaya ya Temeke, Mkoa wa Dar Es Salaam mnamo Machi 8, 2014

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »