March 08, 2014

MJUMBE WA KAMATI KUU YA (CCM) JERRY SILAA AMPIGIA DEBE GODFREY MGIMWA KUCHUKUA JIMBO LA KALENGA

Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na mjumbe wa Kamati kuu ya Chama chama Mapinduzi (CCM) Bw. Jerry Silaa kulia akiteta jambo na Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Bw. Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Ibumila kata ya Mgama halmashauri  ya Iringa vijijini mkoani Iringa, Jerry Silaa amewaomba wana Ibumila na wana Kalenga kwa ujumla wake kumchagua Godfrey Mgimwa ili kukamilisha mipango mbalimbali aliyoiacha  na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Marehemu Dr. William Mgimwa.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KALENGA) 2 
4 
Mmoja wa wananchi akiserebuka huku akiwa amebeba beseni lake la ndizi katika mkutano huo. 5 
Wananchi wakimlaki mgombea ubunge wa Kalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa wakati alipowasili katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama. 9 
Jeshi la polisi likiimarisha ulinzi katika mikutano hiyo 10 
 Kada wa chama cha Mapinduzi Bw. Fredrick Mwakalebela akipigia debe mgombea ubunge wa jimbo la Lalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo leo.
13 
Mgombea ubunge wa jimbo la Lalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa akivishwa mgorole na wazee wa kimila kama ishara ya heshima mara baada ya kuwasili katika  kijiji cha Mgama kata ya Mgama wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo leo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »