March 01, 2014


*KINACHOENDELEA KUTOKA UWANJA WA TAIFA, MECHI BADO MASHABIKI WA SIMBA WARUDIA KUNG'OA VITI
 VURUGU UWANJANI, Mashabiki wa Simba waking'oa viti na kuwarushia mashabiki wa Yanga, kabla ya mchezo wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Yanga na Al-Ahly unaotarajia kuanza muda mchache ujao. 
Vurugu hizo zimeanza baada ya mashabiki wa Yanga kuamua kuzunguka uwanja huo na kusogea hadi eneo la mashabiki wa Simba huku wakishangilia jambo ambalo liliwaudhi mashabiki wa simba ambao waliamua kuanza kurusha chupa za maji na wengine kung'oa viti na kuwarushia mashabiki wa Yanga.
 Mashabiki wa Simba wakirusha viti kuwashambulia mashabiki wa Yanga.
 Wakiendelea kung'oa viti na kurusha
 Mashabiki wa Yanga wakifurahia huku wakionyesha bango lenye idadi ya mabao.
Mashabiki wa Yanga wakishangilia uwanjani.....

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »