KIKOSI
kizima cha Simba SC kinarejea leo Dar es Salaam kwa ndege kutoka
Zanzibar walipokuwa wameweka kambi wiki yote hii kujiandaa na mchezo wa
Nani Mtani Jembe kesho dhidi ya Yanga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Baada
ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar
es Salaam, Simba watakwenda kambini katika hoteli ya Spice, Kariakoo,
Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa kesho.
Taarifa zinasema hakuna majeruhi na wachezaji wote wana ari kubwa kuelekea mchezo wa kesho, unaoandaliwa na wadhamini wa timu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Kilimanjaro. Simba na Yanga zitamenyana Jumamosi katika mchezo wa Nani Mtani Jembe Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, unaoandaliwa na wadhamini wa klabu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
![]() |
| Wanarejea leo; Simba SC wanatua kwa ndege leo kutoka kambini Zanzibar |
Taarifa zinasema hakuna majeruhi na wachezaji wote wana ari kubwa kuelekea mchezo wa kesho, unaoandaliwa na wadhamini wa timu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Kilimanjaro. Simba na Yanga zitamenyana Jumamosi katika mchezo wa Nani Mtani Jembe Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, unaoandaliwa na wadhamini wa klabu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Katika
mchezo huo, utakaochezeshwa na refa Ramadhan Ibada ‘Kibo’ kutoka
Zanzibar, atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Bukoba na Simon Charles
kutoka Dodoma, iwapo dakika 90 zitaisha kwa sare, sheria ya mikwaju ya
penalti itatumika kuamua mshindi.
Viingilio
vya mechi hiyo ni Sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu Sh.
7,000, rangi ya chungwa Sh. 10,000, VIP C Sh. 15,000, VIP B Sh. 20,000
wakati VIP A Sh. 40,000 na tiketi za mchezo huo utakaoanza Saa 10:00
jioni zimeanza kuuzwa leo katika vituo mbalimbali.
Vituo hivyo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
Wachezaji
wanaoruhusiwa kucheza mechi ya kesho ni wale waliosajiliwa ama kikosi
cha kwanza au timu ya vijana pamoja na wapya ambao wameombewa usajili
katika dirisha dogo.
Mara
ya mwisho zilipokutana timu hizo Mei mwaka huu katika mchezo wa Ligi
Kuu, Simba SC ilitoka nyuma kwa mabao 3-0 na kupata sare ya 3-3 Uwanja
wa Taifa.

EmoticonEmoticon