im![]() |
| OKWI MAZOEZINI NA YANGA LEO ASUBUHI |
Baada ya hadithi nyingi za Mwenyekiti wa Simba aliyesimamishwa, Ismail Aden Rage, Okwi ameweka tayari rekodi mbili na Yanga.
Moja ilikuwa
jana alipovaa kwa mara ya kwanza jezi ya Yanga na kupokelewa na viongozi wa
timu hiyo.
Lakini leo, ameweka nyingine baada ya kufanya mazoezi na timu hiyo akiwa chini ya Kocha Mholanzi, Ernie Brandts.
Katika mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar, Okwi alikuwa kivutioo kikubwa na watu wengi walijitokeza kumshuhudia.
Rage amekuwa
akisisitiza Okwi hatocheza Yanga, huenda kesho kauli yake hiyo ikafutika kabisa
atakapoichezea Yanga katika mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba.
Baada ya
mechi hiyo, kitakachosubiriwa ni Okwi kucheza mechi ya mashindano, suala ambalo
Rage atakuwa amepoteza cha kusema.
Rage ameendelea kusisitiza kwamba Okwi hatakiwi kucheza Simba, lakini Yanga wanaendelea na mambo yao kama kawaida.












EmoticonEmoticon