Imewekwa Desemba 20,2013 saa 12:40.
Rubani
wa ndege ya shirika la Ethiopia Airlines iliyotua kwa dharura kwenye
uwanja wa ndege wa Arusha, alitua kwenye uwanja huo baada ya kudhania ni
ule wa Kilimanjaro International Airport (KIA), Mamlaka ya Usafiri wa
Anga Tanzania, (TCAA) imesema.
Badala
yake rubani huyo alitua kwenye uwanja wa ndege wa Arusha wenye njia ya
kutua iliyo na urefu wa meta 1,640 ambayo ni fupi mno kwa ndege hiyo
aina ya Boeing 767-300ER kutua. Ndege hiyo inahitaji walau njia ya kutua
yenye urefu wa meta 1,798.
Mkurugenzi
Mkuu wa TCAA, Fadhil Manongi, alisema kwenye maelezo yake kuwa pamoja
na kwamba kulikuwa na ndege mbovu kwenye njia ya kutua ndege ya KIA,
uwanja huo una njia yenye urefu wa meta 3,600 na kusema kuwa bado
kulikuwa na meta 3,200 zilizotosha kwa ndege No. ET-815 kutua.
SOURCE: TIMES FM

EmoticonEmoticon