Release No. 211
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Desemba 20, 2013
AZAM, SHOOTING TIKETI ZA ELEKTRONIKI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa mechi mbili za majaribio ya
matumizi ya tiketi za elektroniki zitakazochezwa Uwanja wa Azam Chamazi,
Dar es Salaam.
Mechi
ya kwanza itakuwa Desemba 26 mwaka huu saa 10 jioni ambapo
itazikutanisha timu za Azam na Ruvu Shooting. Mechi nyingine itachezwa
Januari Mosi mwakani kwa kuzikutanisha Ashanti United na JKT Ruvu.
TFF
tunatoa mwito kwa washabiki kujitokeza katika mechi hizo ambapo mbali
ya kushuhudia burudani pia watajionea jinsi mfumo huo wa tiketi za
elektroniki unavyofanya kazi.
Kwa
kushirikiana na benki ya CRDB ambayo ndiyo iliyoshinda tenda hiyo ya
tiketi za elektroniki, TFF imepanga vilevile kuandaa mechi nyingine
majaribio mikoani kabla ya mfumo huanza kutumika rasmi Januari 25 mwakani katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
PINGAMIZI DIRISHA DOGO MWISHO DES 23
Desemba
23 mwaka huu ndiyo mwisho wa kipindi cha pingamizi kwa usajili wa
dirisha dogo kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la
Kwanza (FDL).
Katika
VPL, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar na Coastal Union ndiyo timu pekee kati
ya 14 za ligi hiyo ambazo hazikuwasilisha maombi ya usajili katika
dirisha dogo.
Ashanti
United ndiyo inayoongoza kwa wachezaji 15 ambao ni Kassim Kilungo,
Mohamed Banka, Bright Obinna, Victor Costa, Juma Mpongo, Juma Jabu, Ally
Kondo, Shafii Rajab, Mohamed Faki, Abubakar Mtiro, Patrick Mhagama,
Ally Kabunda, Hassan Kabuda, Idd Ally na Rahim Abdallah.
Ruvu
Shooting; Ally Khan na Jumanne Khamis, Rhino Rangers; David Siame, John
Kauzeni, Salum Mamlo, Jingo Seleman, Darlington Enyinna, Rajab Twaha,
Godfrey Mobi na Mussa Digubike. Mbeya City; Saad Kipanga. Tanzania
Prisons; Dennis Liwanda, Godfrey Pastory, Henry Mwalugala, Jamal Salum
na Brayton Mponzi.
Oljoro
JKT; Jacob Masawe, Mansour Ali, Juma Mohamed, Amour Mohamed, Mohamed
Ali, Mussa Nahoda, Benedict Ngasa, Seleman Makame, Shija Mkina, Ali Omar
na Shaweji Yusuf. Simba; Uhuru Selemani, Ivo Mapunda, Ali Badru, Awadh
Juma, Donald Mosoti na Yaw Berko. Azam; Mouhamed Kone.
Yanga;
Hassan Dilunga, Juma Kaseja na Emmanuel Okwi. Mgambo Shooting; Suleiman
Khatib, Bolly Ajali, Amri Sambinga na Issa Ali. JKT Ruvu; Chacha Marwa,
Sino Augustino, Idd Mbaga na Cecil Luambano.
KAMATI YA UTENDAJI TFF DES 23
Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itakutana
Jumapili (Desemba 23 mwaka huu) chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jamal
Malinzi.
Kikao
hicho kitakachofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitapitia ajenda
mbalimbali ikiwemo uundwaji wa vyombo vya haki (Kamati ya Nidhamu,
Kamati ya Maadili na Kamati ya Uchaguzi).
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

EmoticonEmoticon