WAZEE WA NGWASUMA KUWAPAGAWISHA WAKAZI WA MOROGORO.

November 30, 2013

BENDI ya Mziki wa Dansi ya nchini FM Academia “Wazee wa Ngwasuma”inatarajiwa kufanya onyesho kali la Mlipuko wa Burudani mkoani Morogoro  Desemba 6 mwaka huu katika ukumbi wa Kingstone Night Club.

Onyesho hilo linatarajiwa kuanza majira ya saa tatu usiku ambalo litakuwa la aina yake kutokana na aina ya wanamuziki wa bendi hiyo iliyojizolewa umaarufu mkubwa hapa nchini.


Akizungumzia onyesho hilo,Meneja wa Ukumbi wa huo,Juma Abajalo alisema maandalizi yake yanaendelea vizuri ambapo wasanii wa bendi hiyo watawasili mkoa wa Morogoro siku moja lengo likiwa ni kuhakikisha wanakata kiu ya wapenzi wa mziki wa dansi mkoani humo.

Abajalo alisema onyesho hilo linatarajiwa kuwa la aina yake ambapo aliwataka wakazi wa mkoa wa Morogoro kujitokeza kushuhudia burundani ambazo zitapakana siku hiyo ambapo wasanii hao watapata nafasi ya kulitawala jukwaa mahiri litakalokuwa kwenye ukumbi huo maarufu mkoani hapa.

“Ninachoweza kusema maandalizi ya kuelekea onyesho hilo yamekamilika kwa asilimia kubwa hivyo tunawaomba wapenda burudani mkoani hapa kukaa mkao wa kula “Alisema Abajalo.

Abajalo alisema ukumbi huo wa Kingstone Night Club upo eneo la nane nane mkoani humo ambapo wasanii hao wataweza kufanya shughuli ya kuwapa burudani wakazi wa mkoa huo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »