LAAC WAIAGIZA HALMASHAURI HANDENI KUPELEKA ZAIDI YA MILI 105 KWA VIJIJI RUZUKU YA SERIKALI.

November 30, 2013
MWENYEKITI wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Rajabu Mbaruku imeiagiza Halmashauri ya wilaya ya Handeni kuhakikisha kwamba inapeleka kiasi cha sh.milioni 105,779,260 kwa vijiji vilivyostahili kuzipata ikiwa ni michango ya lazima ya asilimia 20 ya ruzuku ya serikakali kuu kwa ajili ya maendelo vijijini,

Kauli ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo ilitokana na halmashauri hiyo kushindwa kuzipeleka vijijini fedha za ruzuku ya serikali kuu kwa ajili ya miradi ya maendeleo hali ambayo inapelekea kuchangia kudhorotesha kasi yao katika shughuli mbalimbali.
Licha ya kutoa agizo hilo pia aliiagiza halmashauri hiyo kuandaa mchanganuo wa madeni inayodai na kudaiwa kwa kuonyesha majina ya wadai na wadaiwa ikiwemo kuchukua hatua za makusudi za kupatikana kwa fedha zinazodaiwa.

Mwenyekiti huyo alisema katika mchanganuo huo wadai wa halmashauri unaonyesha ni kiasi cha sh.milioni 736,302,302 ambapo katika hilo mchanganuo wa wadaiwa hao haukuonyesha kitendo ambacho kinaleta mashaka hasa katika utendaji wake.
Aidha pia kamati hiyo iliagiza mchanganuo wa matumizi ya mabati 466 yaliyotumika kujengea vyumba 8 vya madarasa katika shule ya sekondari Segera uandaliwe na kupelekwa kwa mkaguzi mkazi kwa ajili ya uhakiki zaidi.
Aliitaka halmashauri hiyo kuzingatia vipimo na vigezo vya ubora katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi ambapo agizo hilo lilitokana na kubainika kwa kiwango duni kwa madarasa manne yaliyojengwa kwa sh.milioni 14 katika shule ya sekondari Komnyang’anyo.
Hata hiyo waliitaka halmashauri hiyo kuongeza bidii katika kudai kiasi cha sh.,milioni 133,391,724 ambazo inadai kutoka kwa wadaiwa ambao ni pamoja na MSD sh.milioni 39,310,646,State Business sh.milioni 14,690,000,HADECO sh.milioni 10,200,000, Hazina (15% LAPF) sh.milioni 44,059,300, Hazina(Salaries)sh.milioni 19.806,278 na mfuko wa wanawake ni sh.milioni 5,025,500.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »