NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Coastal Union,Uhuru Seleman juzi
aliweza kuwakonga nyoyo mashabiki wa soka mkoani hapa kutokana na aina ya
uchezaji ambayo alikuwa akiutumia kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya timu yao na
Rhino Rangers ya Tabora.
Mchezo huo ulimalizika kwa timu zote kutoka sare ya
kufungana bao 1-1,uliocheza kwenye dimba la Mkwakwani na kuhudhuriwa na
mashabiki mbalimbali wa soka mkoani hapa.
Uhuru alionekana mwiba hasa baada ya kumiliki mpira kwa
dakika kadhaa huku akitoa pasi nzuri kwa wachezaji wenzake kitendo ambacho
kiliwaacha roho mashabiki wa soka na kuanza kupiga kelele za shangwe.
Akizungumza na Tanga Raha,Uhuru alisema siku zote amekuwa na ndoto ya
kucheza vizuri na kujituma ili kuweza kufanikiwa kurudisha nafasi yake katika
kikosi cha timu ya Taifa na kusema ataendelea kupambana na kumuomba mungu
afanikiwe katika hilo.
EmoticonEmoticon