Na Oscar Assenga,Tanga.
WAPENZI wa Klabu ya African Sports na wanachama wa zamani
wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu ya kuomba uanachama ili waweze
kupata fuksa ya kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wao
utakaofanyika hivi karibuni.
Akizungumza jioni hii na Tanga Raha,Mwenyekiti wa Klabu ya African
Sports “Wanakimanumanu”Asseli Shewally alisema mchakato wa kujaza fomu za
uanachama wa klabu hiyo tayari umeshaanza na fomu hizo zinapatikana makao makuu
ya klabu hiyo barabara kumi na mbili jijini Tanga.
Shewally alisema lengo la kusajili wanachama upya ni katika
kupitisha katiba mpya ili hatimaye kuweza kufanya uchaguzi mkuu wa viongozi
wapya watakaoingoza timu hiyo.
Aidha aliwataka wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi
ili kuweza kuchukua fomu na kurudisha kwa wakati ili kuweza kupata viongozi
watakaoiletea maendeleo timu hiyo.
EmoticonEmoticon