Na Oscar Assenga,Tanga.
WADAU wa soka mkoa wa Tanga wamewashauri wapenzi na mshabiki
wa klabu ya Coastal Union kuwa wavumilivu hasa pale timu yao inaposhindwa
kufanya vizuri katika mechi zao za nyumbani na ugenini badala yake waungane pamoja ili kuitakia mema timu hiyo katika michezo yake ijayo kwenye Ligi kuu Tanzania bara.
Hatua hiyo inatokana na baadhi ya mashabiki wa soka mkoani
hapa kutaka kupaniki katika mechi ya Coastal Union na Rhino Rangers ya Tabora
ambapo mchezo huo ulimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana baoa 1-1,mchezo
uliopigwa uwanja wa mkwakwani.
Akizungumza na blog
hii moja kati ya wadau hao,Msusah Junior alisema suala la matokeo mabaya kwa
timu halisababishwi na mwalimu ila inatokana na aina ya uchezaji wa wachezaji
siku husika kutokana na kuwa kazi kubwa ya mwalimu na kuipa maelekezo timu
kabla ya kuanza mechi.
Naye.Zambi Bakari alisema wachezaji wanapaswa kujituma hasa
pale wanapokuwa mchezo na sio kupaniki kwani kufanya hivyo kunaipelekea timu
husika kushindwa kufanya vizuri na kuwanyima raha wapenzi na mashabiki wao.
Kwa upande wake,Mzee Deo alisema lazima mashabiki wa soka
wafahamu kuwa kuna matokea ya aina mbili kufungwa,kutoka sare na kushinda hivyo
wanapaswa kuridhika na matokeo ya aina yoyote na kuwataka wapenzi na wanachama
kuendeleza mshikamao ili timu hiyo iweza kufanya vema mechi zao zilizosalia
hasa katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu.
Mwisho.
EmoticonEmoticon