PENGO la beki wa kati wa Klabu ya Coastal Union Crispian
Udula limeanza kuithiri timu hiyo mara baada ya jana kuonekana dhahiri kwenye
mechi yao ya Ligi kuu na Rhino Rangers
ya Tabora kwenye mchezo uliocheza kwenye uwanja wa Mkwakwani, uliomalizika kwa
sare ya kufungana bao 1-1.
Udulla alikuwa ni msaada mkubwa katika timu hiyo hasa kwenye
nafasi ambayo alikuwa akiicheza ambapo jana ilionekana kupwaya na kushindwa kutumika
vema kama siku zote.
Mchezaji huyo alishindwa kucheza kutokana na kutumikia adhabu
ya kadi nyekundu aliyeipata kwenye mechi ya Coastal Union na Yanga iliyopigwa
hivi karibuni kwenye uwanja wa Taifa ambapo tayari atakuwa amemaliza adhabu
hiyo na huenda akacheza mechi yao na Ruvu shooting Jumamosi hii.
Udulla ni miongoni wachezaji hatari waliosajiliwa na Klabu
ya Coastal union ya Tanga msimu huu ambapo amekuwa tishio sana kwenye mechi
mbalimbali za ligi kuu akitokea kwenye timu ya Bandari nchini Kenya.
Timu ya Coastal Union tayari imekwisha kucheza nne imeshinda
mechi moja na kutoka sare mechi tatu huku wadau na wapenzi wa timu hiyo
wakiendelea kuiombea mafanikio mema kwenye michezo yao iliyosalia kwenye ligi
hiyo.
EmoticonEmoticon