DC GAMBO KUBARIKI MASHINDANO YA AWESO CUP.

September 20, 2013

NA OSCAR ASSENGA,KOROGWE.
MKUU wa wilaya ya Korogwe,Mrisho Gambo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mashindano ligi ya vijana ya Aweso Cup itayaoanza kutimua  kesho katika uwanja wa soka Mswaha.

Mashindano hayo yamedhaminiwa na Diwani wa Kata ya Mswaha ,Aweso Omari ikiwa na lengo la kuinua vipaji vya wachezaji wachanga na kukuza kiwango cha soka katika kata hiyo ili iweze kuwa na timu tishio siku zijazo.

Akizungumza na blog hii,Mratibu wa Mashindano hayo,Zaina Kassama alisema maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika kwa asilimia kubwa na kueleza tayari timu 10 zimethibitisha ushiriki wao.

Kassama ambaye pi ni Katibu wa Chama cha Soka wilayani Korogwe(KDFA) alizitaja timu shiriki katika mashindano hayo kuwa ni Majengo FC,Cosovo FC,Star FC,Ringstone FC na Mafuleta SC.

Alizitaja timu nyengine kuwa ni Tabora FC,Mswaha Kambini,Mwenga FC,Kwaluma FC na Mandera Lutuba ambazo zitachukua ili kuweza kupatikana kwa bingwa wa mashindano hayo msimu huu wa mwaka 2013.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »