Na Oscar Assenga, Mkinga.
DIWANI wa Kata ya Mkinga (CCM), Juma Maziba amechaguliwa kuwa
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga kwa kipindi chengine mara
baada ya kumshinda mpinzani wake Nassoro Mbaruku wa (CUF) kwenye uchaguzi
uliofanyika juzi kutokana na Makamu huyo kumaliza muda wake kikatiba.
Akitangaza matokeo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,
Cheyo Nkelenge alimtangaza Juma Maziba kuwa mshindi katika nafasi hiyo baada ya
kupata uwa 19 dhidi ya mpinzani wake aliyepata kuwa 9 katika uchaguzi huo kati
ya kura 28 zilizopigwa na wajumbe.
Baada ya kutangazwa matokeo hayo, Maziba aliwashukuru wajumbe
waliomuwezesha kuchaguliwa kwa mara nyengine tena na kuhaidi kuwa mstari wa
mbele kumshauri mwenyekiti wa halmashauri masuala ya kimaendeleo katika wilaya
hiyo kama ilivyokuwa katika awamu yake iliyomalizika.
Alisema ushindi ambao ameupata umempa faraja kuona jinsi gani
anavyokubalika na madiwani wenzake na kuhaidi kuendeleza ushirikiano kwenye
shughuli zao ili kuweza kuchochoa kasi ya maendeleo kwa wananchi wao.
(Picha kushoto ni Makamu Mwenyekiti huyo alipeana mkono na mpinzani wake diwani wa kata ya Moa)
Makamu huyo alichaguliwa katika nafasi hiyo katika kipindi
cha mwaka 2010-2013 kabla ya kuchaguliwa tena kushika wazifa huo ambapo amesema
matarajio yake makubwa ni kushirikiana na viongozi wenzake ili kusukuma kasi ya
maendeleo kwenye maeneo yao.
Mwisho.
EmoticonEmoticon