Na Oscar Assenga, Mkinga.
MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga,Andrew Ngoda
amewataka watumishi wa halmashauri kuepuka kusukumwa na itikadi na hisia zao za kisiasa
,dini,kabila na maeneo yao katika kutekeleza majukumu yao kwani
wanawajibika,kufuatilia na kuratibu utekelezaji wa maamuzi ya halmashauri kwa
kuzingatia mtiririko wa uongozi.
Ngoda ametoa kauli hiyo leo wakati wa kikao cha Baraza la
Madiwani ambacho kilikuwa kwa ajili ya madiwani kuwasilisha taarifa za miradi
ya maendeleo kwenye kata zao kabla ya kufanyika kikao kingine kesho.
Mwenyekiti huyo amesema maadili yanaweza kuwasukuma madiwani
kuheshimu nafasi na hadhi madiwani wenzao hali kadhalika watumishi wa
halmashauri wazingatie kwa kiwango cha juu uadilifu kwa kuzingatia sheria,
kanunu na miongozo ya utawala bora katika utendaji wao.
Ameongeza kuwa watumishi wa ngazi zote baadhi wanaanguka sana
kwenye uwazi na uwajibikaji ambapo amewataka kuelewa kuwa uwazi ni kufanya
jambo bila kificho na uwajibikaji ni kuwasilisha taarifa ya dhamana ya utendaji
wao kwa aliyekupa dhamana.
Aidha amewaeleza kuwa uwajibikaji ni msingi wa utawala bora
ambao unawataka watumishi katika ofisi za umma kuwajibika kwa matendo yao ili
kuleta imani kwa wananchi wanaowaongoza katika maeneo husika.
Ameeleza kuwa uwazi unawezesha uelewa na ufuatiliaji wa
mchakato ili kujua kama unaendeshwa kwa kuzingatia misingi ya sheria na kanuni
zake na kufikia malengo yaliyotarajiwa kufikiwa na kueleza uwajibikaji,uwazi
vyote viwili ni muhimu katika kusaidia matumizi sahihi bora kwenye kuendesha
masuala ya halmashauri na nchi katika ngazi zote.
Hata hivyo amesisitiza utawala bora kwenye maeneo yote
uzingatiwe hivyo kwa vile fedha zinapatia kwenye kitengo cha manunuzi ambapo
amewataka kuzingatia mpiango sahihi, nyaraka sahih, kuwahi katika kuitisha
zabuni, ufanisi na kutenda haki na kutenda haki katika mchakato wa tathimini za
zabuni.
Mwisho.
EmoticonEmoticon