Jumla ya Nyumba 12 zilizokuwa zimejengwa na wahamiaji haramu
jamii ya wafugaji ndani ya hifadhi ya
msitu wa Msububwe wilayani Pangani Mkoani Tanga zimeteketezwa kwa moto na
kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ikiwa ni katika oparesheni ya
kuondosha wavamizi wa hifadhi hiyo .
Zoezi hilo ambalo linalenga kulinga hifadhi ya msitu huo
dhidi ya wavamizi hao wa kabila la
wamang”ati ambao walikuwa wamevamia hifadhi na kuanza kufanya uharibu wa kuharibu vyanzo vya maji, kukata miti hovyo ya kujengea nyumba , kuni
pamoja na kuchunga mifugo yao.
Akiongea na gazeti hili wakati wa oparesheni hiyo Kaimu
Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Pilika Kasanda alisema zoezi hilo litakalo dumu
kwa muda wa siku tano la kuwamisha na
kuharibu makazi ya wavamizi hao ili kulinga
hifadhi hiyo isiendelee kuharibiwa.
“Zoezi hili limeanza leo na litadumu kwa siku tano katika
kukagua na kuwaondosha kwa nguvu wavamizi wote wafugaji walioko ndani ya
hifadhii kwani wameanza uharibu wa vyanzo vya maji ambavyo ndio tegemeo pekee
la wilaya hii”alisema Kasanda.
Alisema wafugaji ho
wamekuwa wakivamia msitu huo mara kwa mara licha ya juhudi mbalimbali
walizozichukuwa za kuwapa elimu kuhusu umuhimu wa hifadhi hiyo na kuwataka
warudi katika makazi yao ya awali lakini imeshindikana.
Hata hivyo Meneja hifadhi msitu huo John Mkenda alisema
kabla ya zoezi hilo walianza kutoa elimu kwa jamii inayozunguka hifadhi kuhusu umuhimu wa
hifadhi hiyo na madhara ya uharibufu unaofanyika ili kuhakikisha wanalinda
hifadhi na viumbe vilivyoko.
“Tulianza kutembelea vijiji vinavyozunguka hifadhi ili kutoa
elimu ya mazingira kisha tukawatembelea na wavamizi ambao ni jamii ya wamasai na
kuwashauri watoke kwa amani kabla ya hatua za kisheria kuanza kufuatwa ,tunashukuru
walitii ili wengine walikaidi”alisema Mkenda.
Aliongeza kuwa nyumba nne hawakuzichoma moto kutoka na
kutowakuwa wazazi bali wapo watoto pekee lakini nao wamewapa siku mbili
kuondoka kwa hiari kabla ya kuanza kuchoma moto nyumba hizo pamoja na vitu
vyao.
MWISHO
EmoticonEmoticon