Na Oscar Assenga, Tanga.
SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo imeshauriwa
kuweka utaratibu wa kukaa na makocha wa kigeni wanaofundisha timu za Taifa muda
mrefu ili kuweza kupata mafanikio badala ya kuwabadilisha kila wakati kitendo
ambacho kinadumaza soka badala ya kupiga hatua kwenda mbele.
Ushauri huo ulitolewa na Golikipa wa zamani wa timu ya Coastal Union ya
Tanga, Nyendi Mpangala wakati akizungumza na mwandishi wa blog hii hivi karibuni ambapo alisema kitendo cha ubadilishwaji wa makocha hao
kunawafanya hata wachezaji wenyewe kutokuelewa kile wanachofundishwa kutokana
na kila kocha mpya anakuwa na mbinu zake.
Nyendi aliwahi kuichezea Costal Union ya Tanga kati ya mwaka 2000-2003
alipoamua kuacha kujishughulisha na mambo ya soka hapa nchini na kueleza mpira
wa sasa hivi ni tofauti na zamani kutokana na enzi hizo wachezaji wengi
walikuwa na vipaji vyao binafsi kuliko ilivyokuwa wakati huu .
Alisema ili soka letu hapa nchini liweze kupiga hatua ni lazima serikali
ihakikishe wanahamasisha wadau kuanzisha vituo vya mafunzo ya soka (Academy)
ambazo zitakuwa imara kwa ajili ya maendeleo ya soka hapa nchini ikiwemo
kuvilinda vipaji hivyo pamoja na kulinda viwanja vya michezo vilivyopo maeneno
mbalimbali na kuwapa fuksa wachezaji kucheza.
Akizungumzia nafasi ya mlinda mlango alisema ni ngumu lakini ni rahisi
endapo wachezaji wenyewe wataipenda kutokana na kuwa nafasi ambayo mara moja
unaweza kupata nafasi ya kwenda kucheza kwenye timu nyengine ikiwemo timu ya
Taifa kwa sababu ni mahali ambapo mtu anaonekana.
Mwisho.
EmoticonEmoticon