Na Oscar Assenga, Tanga.
UFINYU wa Bajeti wa maeneo salama ya uwekezaji ambayo
yatahakikisha urejeshaji wa mtaji na kupata faida kwa wakati uliokusudiwa ni
miongoni mwa changamoto ambazo zinaukabili mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa
Umma PSPF mkoa wa Tanga.
Meneja wa Mfuko huo Mkoani hapa, Salome Makalla aliyasema
hayo wakati akitoa Mada kwa wafanyakazi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga hivi
karibuni ambapo alisema changamoto nyengine ambayo wanayokabiliana nayo ni
ongezeko la mfumuko wa bei unaosababisha kukosekana kwa faida hali na hivyo
kuathiri thamani ya fedha iliyowekezwa.
Makalla alisema kuwa suala lengine ambalo limekuwa kikwazo
kikubwa kwao ni kukosekana kwa nyaraka muhimu wakati wa kuomba mafao imekuwa
ikiathiri wastaafu kwakuwa mapungufu hayo husababishwa kuchelewa kwa malipo na
hivyo kushindwa kumudu mahitaji ya kila siku baada ya ustaafu kazi.
Alisema licha ya kumuathiri mstaafu pia mfuko umekuwa
ukiathirika kwa kushindwa kutimiza lengo lake la kulipa mafao kwa wakati.
Aidha alisema mikaati yao ya baadae ni kuviwezesha vikundi
vya kuweka aiba na kukopa Saccos vya wanachama ambapo mfuko unafanya tathimini
ya namna bora ya kuviwezesha vikundi hivyo kujiendesha na kukopesha wanachama
wake zaidi kwa wingi.
Aliongeza kuwa mfuko unatarajia kuwa unavikopesha vikundi
hivyo kwa riba nafuu ili viweze kuwapatia mikopo ya kujiendeleza wanachama wao
ambapo pia ni wanachama wa mfuko wa PSPF.
Mwisho.
EmoticonEmoticon