Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amempigia simu Waziri wa Ujenzi Ndugu. Innocent Bashungwa na kumtaka kuongeza nguvu katika kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Kakonko kuelekea Halmashauri ya Kakonko yenye urefu wa Kilomita 3 kwa kiwango cha lami ambapo Waziri Bashungwa ameahidi kutekeleza ili wananchi kuondokana na changamoto hiyo ya mawasiliano.
Akiwa Wilayani Kakonko, Mwenezi Makonda amepokea changamoto hiyo ambapo aliwataka TANROADS na TARURA kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa kuzingatia muda ilikusudi Watanzania kunufaika na urahisi wa mawasiliano ya barabara kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa haraka.
Pia, Amewasihi watendaji kuongeza nguvu ya ushawishi ili kupata fedha za kutekeleza miradi kwa haraka.
“Ahadi za Rais ni ahadi ya upendeleo na sio maana kwamba mipango iliyopo inaachwa..Hapana, ndio maana tunatekeleza Bajeti kwa kutekeleza Ilani ya CCM na maelekezo ya Viongozi wakuu” Alisema Mwenezi Makonda.
“Kwenye Maendeleo kazi kubwa tuliyonayo ni uwezo wa ushawishi, Keki inaweza kuwa ndogo lakini ni nyinyi namna gani ya kuipambania, Wataalam ongezeni namna ya ushawishi kutekeleza na kukamilisha miradi ya maendeleo Nchini” Amesema Makonda.
EmoticonEmoticon