WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII NI TEGEMEO KATIKA SEKTA YA AFYA

February 01, 2024

 Na. WAF - Dar Es Salaam


Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ndio Mstari wa mbele katika Sekta ya Afya wanaoweza kuibua wagonjwa na kutoa taarifa zote kuhusu masuala ya Magonjwa ikiwemo yasiyoambukiza na yakuambukiza kama ya milipuko.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Januari 31, 2024 wakati wa Uzinduzi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii iliyozinduliwa leo na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdori Mpango katika kituo cha Mkutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam.

''Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii ndio askari wa mbele katika Sekta ya Afya na ndio wanaibua wagonjwa na wanaweza wakazuia na kutoa taarifa zote kuhusu masuala ya magonjwa na ni nguzo muhimu katika kuimarisha mifumo ya Afya ngazi ya jamii ili kufikia lengo la huduma za Afya kwa wote.” Amesema Waziri Ummy

Aidha, Waziri Ummy amesema Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wanaenda kuwapunguzia mzigo watumishi walio katika ngazi za Hospitali kwa kuwa kuna baadhi ya vijiji havina vituo vya Afya au vinapatikana mbali na makazi ya watu.

“Ndio maana tumeona ni muhimu sasa turasimishe mpango huu ili kutomuacha mtu yoyote, Mfano kwa upande wa ugonjwa wa Kifua Kikuu tulipoamua kutumia wahudumu wa Afya ngazi ya jamii wameibua wagonjwa wapya asilimia 50 kwa kila wagonjwa wapya 100 wanaogunduliwa na ugonjwa huo."  Amesema Waziri Ummy.







Share this

Related Posts

Previous
Next Post »