Na Eleuteri Mangi, WANMM
Wadau wa sekta mipango miji wamekutana Jijini Dodoma kujadili rasimu ya marekebisho ya Kanuni za Sheria za Mipango Miji nchini ili ziendane na mabadiliko ya kasi ya ukuaji miji pamoja mchango wake wa sekta hiyo katika hafua muhimu za kuifadhi mazingira.
Akifungua kikao hicho Januari 30, 2024 jijini Dodoma, Naibu Katibu Wizara ya ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Lucy Kabyemera amesema kuwa ardhi inahitaji kupangwa, kupimwa, kumilikishwa na kuendelezwa ikiwa katika hali nzuri kiuchumi, kijamii na kimazingira.
“Natambua ili kufanikisha azma hii, tunahitaji kuwa na kanuni sahihi za kuongoza upangaji wa miji yetu pamoja na matumizi mbalimbali ya ardhi hapa nchini” Naibu Katibu Bi Kabyemera.
Wadau hao ni pamoja na Manejimenti ya Wizara, Makamishna wa Ardhi Wasaidizi kutoka mikoa ya Tanzania Bara, wawakilishi kutoka Wizara mbalimbali, taasisi za Serikali pamoja na zisizo za Serikali.
EmoticonEmoticon