WAZIRI MAVUNDE AIPONGEZA BODI, MENEJIMENTI KWA KUING’ARISHA STAMICO

January 30, 2024



Waziri ya Madini, Mhe.Anthony Mavunde,akiipongeza Bodi ya Wakurugezi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),mara baada ya kufanya kikao cha pamoja na bodi hiyo kilichofanyika leo Januari 30,2024 jijini Dodoma.



Waziri ya Madini,Mhe. Anthony Mavunde,akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na Bodi ya Wakurugezi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kilichofanyika leo Januari 30,2024 jijini Dodoma.



Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO, Meja Jenerali Mstaafu Micheal Isamuhyo,akizungumza wakati wa kikao cha Waziri ya Madini, Anthony Mavunde na Bodi ya Wakurugezi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kilichofanyika leo Januari 30,2024 jijini Dodoma.


Waziri ya Madini,Mhe. Anthony Mavunde,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao cha pamoja na Bodi ya Wakurugezi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kilichofanyika leo Januari 30,2024 jijini Dodoma.

Na Gideon Gregory Dodoma.

Waziri ya Madini,Mhe. Anthony Mavunde,ameipongeza Bodi ya Wakurugezi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kwa kuendelea kukuza sekta ya madini nchini kwa kununua mitambo mikubwa ya kuchoronga miamba pamoja na kuwasaidia wachimbaji wadogo kukua.

Waziri Mavunde ametoa pongezi hizo leo Jijini Dodoma Januari 30,2024 alipokutana na Bodi ya Wakurugezi ya STAMICO na ambapo amesema kuwa shirika hilo limekuwa liking’ara zaidi na kuwa moja kati ya mashirika ya umma yaliyopiga hatua kiasi cha kutoa gawio la bilioni 8 kwa serikali.

“Nitumie nafasi hii pia kuipongeza menejimenti ya shirika hili pamoja na wafanyakazi wake kwa kufanya kazi kwa bidii na kuliwezesha shirika lenu kuongeza mapato yake kutoka billion 1.4 hadi billion 61 kwa kipindi cha miaka minne iliyopita,”amesema.

Aidha amesema kuwa kazi kubwa imefanyika kuhakikisha STAMICO inafufuka kutoka kuwa moja ya mashirika yaliyotakiwa kufutwa hadi kuwa moja ya mashirika yenye tija kwa Taifa.

“Serikali sasa tunajivunia utendaji mzuri wenye tija wa shirika hili. Naipongeza bodi, menejimeti na wafanyakazi wa STAMICO kwa kazi nzuri mnayoifanya,” amesema Mavunde.

Aidha Waziri Mavunde amesema kuwa shirika la madini Tanzania STAMICO linao uwezo mkubwa wa kutatu tatizo la umeme nchi kwa ajili ya kuwagusa watanzania

“STAMICO kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati anaamini wakishirikiana wanaweza kuwasaidia Watanzania kupata umeme wa uhakika.”amesema

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO, Meja Jenerali Mstaafu Micheal Isamuhyo amemshukuru Waziri Mavunde pamoja na uongozi mzima wa wizara kwa jinsi wanavyoshirikiana na shirika hilo katika mambo mbalimbali katika kuiletea maendeleo nchi pamoja na wizara hiyo.

Pia amemuahidi waziri huyo kutekeleza maagizo yote aliyowapatia hasa ikizingatiwa yanalenga kuendeleza sekta ya madini nchini.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »