Sehemu ya Vifaa hivyo
Na Oscar Assenga, KOROGWE.
Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) limetoa msaada wa vifaa vya tehama katika
Hospitali ya Mji wa Korogwe ya Manundu na kuweka miundombinu ya Intaneti,Ufugaji wa Mfumo
wa kieletroniki ambao ni mfumo wa taarifa za usimamizi wa Hospitali za Serikali
ya Tanzania (GoTHOMIS) pamoja na kufanya mafunzo endelevu kwa watumishi.
Alisema kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani ambao ni wafadhili wao lakini pia wameshirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya pamoja na Ofisi ya Rais Tamisemi wamekuwa wadau kwa mkoa wa Tanga kwa miaka tisa kwa awamu ya miaka mitatu mitatu.
Msoffe alisema kuwa mara nying wamekuwa kwenye awamu uliyoanza
mwaka 2023 na itakwenda mpaka 2026 kwa mkoa wa Tanga na wana jumla ya
Hospoitali 18 wanazozisaidia lakini katika eneo la Tehama pamoja na kwamba
huyko nyumba wamefanya kazi na Hospitali nne kwenye eneo hilo lakioni
watawasapoto kuweka miunbdombi na kuwafanya mafunzo watumishi waweze kuutumia.
“GIZ inaipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuweka mazingira bora ya kisera na kutoa msaada wa kitaalamu katika kuboresha huduma za afya chini Tanzania”Alisema.
Alisema maboresho hayo yanayoendelea katika mifumo ya kidigitali
na hasa mfumo wa GOTHOMIS ambao ni moja ya mifano tosha ya dhamira ya Serikali
ya Tanzania katika kusaidia vituo vya afya kuboresha huduma za afya kupitia
teknolojia ya kidijitali.
Kwa hiyo hospitali ya Korogwe imejitolea kutumia maendeleo ya
kidijitali ili kutoa huduma ya hali ya juu kwa wateja wake. Kuachana na
matumizi ya makaratasi na kuharnia mifumo ya kidigitali ni tatua muhim katika
kufikia lengo hili.
Awali akizungumza Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mji wa Korogwe Dkt Heri Kilwale alisema kuwa kubadilika kutoka matumizi ya karatasi na kutumia mifumo ya kidijitali itawasaidia watoa huduma za afya kuweza kupata taarifa za mgonjwa kwa wakati na salama.
Alisema pia kutapunguza muda ambao wafanyakazi hutumia kufanya kazi za kujaza makaratasi mengi na hivyo wataalamu wa afya wataelekeza zaidi muda katika kutoa huduma kwa wagonjwa na hivyo kupelekea kuongezeka kwa ubora wa huduma zinazotolewa.
Korogwe ni miongoni mwa hospitali chache ambazo zimeanza kutumia
toleo jipya la GoTHOMIS na kva msaada wa mara kwa mara kutoka kwa serikali,
ongozi wa hospitali na washirika wa maendeleo, inatarajiwa kuwa hospitali ya
Korogwe itafanikiwa katika dhamira yake ya mabadiliko kutoka matumizi ya
karatasi Kwenda katika mifumo ya huduma za kidijitali na kwamba. Serikali
itapanua msaada huo kwa hospitali zingine baada ya hapo.
EmoticonEmoticon