WATEKAJI WATATU WA WATOTO GEITA WADAI MILIONI 4 KUWAACHIA

January 19, 2024


 Watu watatu wanashikiriwa na Jeshi la Polisi Mkoani Geita kwa tuhuma za kuteka watoto maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Geita ikiwemo Halmashauri ya wilaya ya Geita kwa lengo la kujipatia kipato.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita ACP .Safia Jongo amesema kumezuka wimbi kubwa la utekaji watoto Mkoani humo ambapo Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao huku chanzo kikitajwa ni kutaka kujipatia Fedha.

“Lakini pia limeibuka wimbi la wizi wa watoto Geita vyanzo ikiwa ni kipato tuna tukio ambalo limetokea mbogwe Mtoto wa Miaka 4 Ametekwa waliomteka wakadai Milioni 4 lakini ndani ya siku tatu Jeshi la polisi tumepambana na tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu ambao walishirikiana kumteka huyo mtoto, ” ACP. Jongo.

Aidha ACP. Jongo amewatahadharisha wazazi na walezi kuhakikisha wanawalea watoto na kuwajengea mazingira Mazuri ya kimalezi ili kukabiliana na wimbi hilo ambalo limeibuka ndani ya Mkoa wa Geita huku akitoa tahadhali na kuwaonya waganga wa kienyeji wanaopiga ramli chonganishi kuwa washirika wakubwa wa Matukio hayo.

ACP. Jongo amesema Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na wananchi katika kupunguza wimbi la Mauwaji ndani ya Mkoa wa Geita ambalo limekuwa likichangiwa na Imani za Kishirikina .


Chanzo :Milladayo

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »