“UDHAMINI WA LIGI YA KIKAPU MKOA TANGA WAIPASUA KICHWA TRBA

April 06, 2018
CHAMA cha Mpira wa Kikapu Mkoani Tanga (TRBA) kimeanza kusaka wadhamini ambao watafanikisha michuano ya ligi ya mkoa itakayoanza hivi karibuni Jijini Tanga ikishiriki timu kutoka wilaya mbalimbali.

Hayo yalibainishwa na Katibu Msaidizi wa Chama hicho, Patrick Semindu wakati akizungumza na Tanga Raha Blog ambapo alisema wameamua kufanya hivyo mapema ili kuweza kufanikisha malengo yao ya kuchezwa mashindano hayo.

Alisema pia kutokana na kuwepo kwa changamoto kamati ya ufundi na utendaji itakutana mwishoni mwa wiki hii kuweza kuweka mipango itakayosaidia kupatikana udhamini ambao utasaidia kuendesha mashindano hayo.

“Kikao hicho kitakuwa na agenda mbalimbali ikiwemo kuidhinisha tarehe ya kuanza mashindano hayo na namna yatakayoendeshwa lakini mpaka sasa hakuna mdhamini yoyote aliyekwisha kujitokeza kama tukikosa tutaendesha ligi kupitia ada za timu shiriki “Alisema

Hata hivyo alisema lengo la kufanya hivyo iwapo wadhamini watakosekana ni kuhakikisha michuano hiyo inafanyika kwa namna yoyote ile na bingwa wa mkoa aweze kupatikana.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »