SHIRIKA LA AGPAHI LAKABIDHI MASHINE YA KUCHUNGUZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WANAWAKE KWA WILAYANI MUHEZA

March 23, 2018




Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa kushoto akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Muheza MwanashaTumbo mashine ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake(cryotherapy machine) kushoto anayeshuhudia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Dkt Asha Mahita


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa akimpongezwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo mara baada ya makabidhiano hayo kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Dkt Asha Mahita



Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa katikati akiwasikiliza kwa umakini Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita na kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Monica Kinala

SHIRIKA la AGPAHI linalojihusisha na masuala ya ukimwi katika kutambua mchango wa sekta ya afya katika ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza limemkabidhi mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanaasha Tumbo mashine ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake( cryotherapy machine).

Mashine hiyo mkuu wa wilaya ya Muheza alikabidhiwa juzi na mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katika warsha ya siku mbili ya wadau wa sekta ya ukimwi kutoka taasisi binafsi na serikali iliyofanyika katika ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga juzi.

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo hiyo Dr.Sekela Mwakyusa alisema kuwa katika kutambua mchango wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mkuu huyo wa wilaya ya Muheza katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza waliamua kumzawadia mashine hiyo ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika vifaa tiba.

"Sisi AGPAHI leo tunakukabidhi mashine hii ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kama sehemu ya mchango wetu katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza" alisema Mwakyusa.

Kwa upande wake mkuu huyo wa wilaya alilishukuru shirika hilo hiyo kwa kumzawadia kifaa hicho muhimu ambapo kwa kuanza atakikabidhi katika hospitali Teule ya Muheza( Muheza DDH) ili ianze kazi.

Hata hivyo aliwashukuru shirika la AGPAHI kwa kunipatia kifaa hiki muhimu kwa wakina mama,nikisema kikae mpaka hospitali ikamilike kitaharibika hivyo nitawakabidhi hospitali Teule ya Muheza ili waanze kukitumia" alisema.

Kwa kuanzia mkuu huyo wa wilaya alimuomba mganga mkuu wa mkoa kupanga siku maalum ya upimaji wa saratani ya kizazi wilayani Muheza ili wakinamama wote wa mkoa wa Tanga wapate huduma hiyo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »