Naibu katibu mkuu bara wa umoja wa wanawake wa
chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele akiongea na wananchi pamoja na wanachama wa chama cha mapinduzi Tarafa ya mazombe wakati wa ziara ya viongozi wa UWT taifa akiwa sambamba na viongozi wa umoja huo mkoani Iringa
Naibu katibu mkuu bara wa umoja wa
wanawake wa
chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele akiwapatia kadi wanachama wapya wa umoja wa chama cha mapinduzi Tarafa ya mazombe wakati wa ziara ya
viongozi wa UWT taifa akiwa sambamba na viongozi wa umoja huo mkoani
Iringa
Naibu katibu mkuu bara wa umoja wa
wanawake wa
chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele pamoja
na wanachama wa chama cha mapinduzi Tarafa ya mazombe wakati wa ziara ya
viongozi wa UWT taifa akiwa sambamba na viongozi wa umoja huo mkoani
Iringa wakiwasindikiza wanachama wapya kula kiapo cha kukitumikia chama hicho
Katibu
wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer akiwaonge na wananchi pamoja na wanachama wakati wa ziara ya viongozi wa UWT taifa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
NAIBU
katibu mkuu bara wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva
Kihwele amevuna wanachama wapya zaidi ya mia tatu
(300) katika tarafa ya Mazombe wilayani Kilolo mkoani Iringa ambo wamejiunga
rasmi na umoja huo.
Wanachama hao wamepokelewa wakati wa ziara ya viongozi wa ngazi
za juu wa UWT taifa mkoani Iringa, ambapo naibu
katibu mkuu bara Eva Kihwele alipokuwa akiongea na
wanachama pamoja na wananchi wa tarafa ya Mazombe ndipo waliposhawishika
kujiunga na umoja huo kutokana na hamasa walioipata kutoka kwa katibu huyo.
Kihwele alisema kuwa chama cha mapinduzi ni chama ambacho
kimejengwa kimisingi ya kulea jumuhia mbalimbali ambazo zipo ndani ya
chama hicho ndio maana bado kinanguvu katika siasa za hapa nchini hata kimekuwa
mfano kwa nchi nyingine.
“Jumuiya ya umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi Tanzania ni
moja kati ya jumuiya ambayo ipo ndani ya chama hiki na inakazi zake kwa ajili
ya kukijenga chama na kuleta maendeleo kwa wananchi waliokipa dhamana ya
kuongoza nchi hii” alisema Kihwele
Aidha Kihwele aliwataka wanawake kujifunza kujifunza kujitegemea ili
waweze kuja kuwaajiri wanaume ambao kwa sasa ndio wamekuwa wakitoa ajira nyingi
kwa wanawake hapa nchini.
“Wanawake wenzangu sasa imefika mwisho wa kuwa tegemezi kwa
wanaume inatakiwa sasa tusimame sisi kama sisi na tuanze kuwaajiri na kulisha
wanaume zenu majumbani kwetu maana tunauwezo wa kufanya kila kazi hizo
inatakiwa tujitume” alisema Kihwele
Kihwele alisema kuwa wanawake mkiwa mnataka kufanya biashara
zenye malengo msiogope kwenda kukopa maana siku hizi kuna mikopo ya bei rahisi
na riba yake sio kubwa ambayo itakuwezesha kufanya biashara yako kwa maendeleo
yako.
“Siku hizi kuna mabenk mengi yanawakopesha wanawake na
wanawaamini sana wanawake kwenye kufanya biasha hivyo nendeni mkakope msiogope
maana hizi benk zipo kwa ajiri ya kusaidia kuinua maisha ya mtanzania” alisema Kihwele
Kihwele alimalizia kwa kuwataka wanawake wa kata ya Mkwawa
mkoani Iringa kuzitumia pesa kwa nidhamu ya hali ya juu ili ziweze kuleta
matunda ya kuleta maendeleo ambayo yanahitajika kwa maisha yao.
“Jamani kila pesa ukiitumia kwa nidhamu basi utaona faida yake
na itakuletea maendeleo yako na taifa kwa ujumla maana unakuwa umetumia vizuri
pesa kwa maendeleo” alisema Kihwele
Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia
chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve alisema kuwa atawapatia elimu ya
ujasiliamali ili wakipata mitaji waweze kuitumia vizuri kwa ajili ya manufaa ya
maendeleo.
“Jamani mimi nimekuwa nikitoa elimu ya ujasiliamali mara kwa
mara kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya biashara zenu kwa faida na kutoa
elimu ya matumizi ya fedha hivyo nawaomba nikiitisha tena kutoa elimu mkaribia
kwa wingi maana huwa inakuwa bure” alisema Twelve
Naye Katibu
wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer amewataka wanawake kote nchini
kujikwamua kiuchumi kwa kufanya shughuli ndogo ndogo za ujasiriliamali ili
kuachana na utegemezi.
Laizer
alisema kuwa baadhi ya wanawake hasa wa vijiji wamekuwa wakipata msongo wa
mawazo kutokana na kutokuwa na kipato licha ya kushiriki shuhuli za uzalishaji
mali ngazi ya familia lakini wengi wao wamekuwa hawashirikishwi katika matumizi
ya kipato walichokitolea jasho.
Laizer
alisema kuwa kuna mifuko maalumu ya kuwaisidia wanawake hasa wa hali ya
chini kwa kuwapatia mitaji kupitia vikundi ili kuanzisha biashara ndogo
ndogo na kuachana na utegemezi hivyo msaada walioupata utawafanya wapige hatua
kubwa zaidi.
Laizer
alisema kuwa kumsaidia mwanamke wa hali ya chini kwa kumuwezesha kimtaji ni
kukomboa jamii kwani mama huyo ataweza kuhuduma familia yake bila ya kuwa
tegemezi.