SHEHENA YA BIDHAA YAKAMATWA WILAYANI MUHEZA

March 23, 2018
 Sehemu ya Shehena ya sukari iliyokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tanga
 Sehemu ya Mafuta ya kula yaliyokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tanga wakati wa operesheni yao
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Edward Bukombe kulia akiwaonyesha waandishi wa habari shehena ya sukari iliyokamatwa
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Edward Bukombe akiwaonyesha shehena ya sukari iliyokamtwa waandishi wa habari ambao hawapo pichani
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Edward Bukombe akionyesha pia baadhi ya vitu vilivyokamatwa

JESHI la Polisi Mkoani Tanga kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato wam ekamata shehena ya bidhaa kwenye kisiwa cha Karange karibu nabandari bubu ya Kigombe wilayani Muheza huku watu watano wakishikiliwakwa kuhusika kuingiza bidhaa hizo.

Bidhaa hizo zilikuwa zikiingizwa kwa kutumia usafiri wa majahazi  ni sukari na mafuta zimekamatwa kufutia operesheni ambazo Jeshi la Polisi wanaloendelea nalo kwa nchi kavu na majini kuhakikisha wanazibiti biashara haramu ya magendo kuingia mkoani hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Edward Bukombe alithibitisha kukamatwa kwa shehena hiyo juzi na watu hao ambao wanadaiwa kuhusika na usafirishaji wa magendo kwa njia ya bahari.

 Alisema ukamataji wa bidhaa hizo unatokana na operesheni za nchi kavu na baharini zinazoendelea kupitia jeshi hilo ili kudhibiti wimbi la uingizwaji wa bidhaa za magendo zinazoingizwa mkoani hapa kupitia bandari bubu.

Kamanda Bukombe alisema kuwa majahazi hayo yalikuwa yamesheheni mifuko 300 ya sukari,madumu 200 ya mafuta ya kula na vitambaa vya kushonea nguo za wakina nama maarufu kama majora vikiwa vinatokea katika visiwa vya Zanzibar na Pemba.

Alisema jeshi hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vitaendelea kufanya operesheni zake ili kuhakikisha wafanya biashara wote wanatumia bandari zilizorasimishwa kwa ajili ya kuingizia bidhaa zao kihalali na kuzilipia kodi.

“Tunamashaka na watu hawa na hata hizi bidhaa zenyewe maana kama kweli hazina mashaka kwa nini wanaziingiza kwa njia ya panya zinaweza kuwa hazina ubora au watu hawa wanakwepa kodi sisi tutapambana nao tu”Alisema.

Bukombe alisema hatua ya kukamata ni ya awali na kukabidhi bidhaa hizo kwa mamlaka ya chakula na dawa ili wathibitishe ubora na mamlaka ya mapato Tanzania watatoa maamuzi ya bidhaa hizo na vyombo vilivyo bebea.

Alisema watuhumiwa wote wapo chini ya ulinzi mkali na hakutaja majina yao mapema kwa ajili ya swala la kiupelelezi na kusema baada ya kukabidhi taarifa kamili katika mamlaka husika taariza itatolewa kwa hatma ya bidhaa hizo na vyombo.

Akizungumzia ukamataji huo mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Kigombewilayani Muheza Athumani Mbwambo alisema ipo haja kwa serikali kuangalia upya suala la kodi ili kuepusha wafanyabiashara kuendelea kutumia njia za panya  na kujikuta wakiingia mikononi mwa Polisi na kupoteza mitaji yao.

Alisema pamoja na ukamataji huo lakini serikali iweka mpango mzuri wa kuzirasimisha bandari bubu za asilimia ikiwemo ya Kigombe ili kuwawezesha wafanyabiashara wanaoitumia kulipa kodi.

“Lakini pia nafikiria Serikali inaowajibu wa kuangalia upya kodi
wanazotoza inawezekana zikawa kubwa kuliko mitaji yao na kupelekea wafanyabiashara kukwepa kutumia njia halali”Alisema.

Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »