WANAWAKE WATAKIWA KUCHANGAMANA ILI WAWEZE KUJIKWAMUA KIUCHUMI

March 17, 2018
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Tantrade Tanzania,Jacqueline Maleko akizungumza wakati wa usiku wa Wanawake na tunzo kwa Mwanamke aliyefanikiwa kwa mwaka 2018 iliyoandaliwa na Tasisi ya Shangwe ambapo wanawake kutoka sehemu mbalimbali walikutana na kuzungumza mambo ya ujasilimali na namna ya kuvuka kutoka hatua moja hadi nyingine.
 Mkurugenzi wa Tasisi ya I-learn East Afrika ,Noela Bomani(Kulia) Akikabidhi tunzo kwa Mwanamke aliyefanya vizuri na kuwa kivutio katika mafanikio yake katika kipindi cha mwaka 2017/2018 Joyce Ibengwe ambaye ni mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko  Kutoka kwa Tasisi ya waajiri nchini(ATE).
 Mshindi wa Tunzo ya Mwanamke aliyefanikiw akwa mwaka 2017/2018 Joyce Ibengwe ambaye ni mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko  Kutoka kwa Tasisi ya waajiri nchini(ATE).akizungumza namna alivyopitia mpaka kufikia hatua hiyo kutoka kuitwa mama na watu mpka mke wa mtu.
 Meneja Bima ya magari kutoka shirika la Bima ya Taifa (NIC) Emakulata Mwaitege, akizungumza umuhimu wa Wanawake kujiwekea bima katika biashara zao na maisha yao hili waweze kusimama tena pindi majanga yanapowakuta.
 Mkurugenzi wa Tasisi ya I-learn East Afrika ,Noela Bomani akieleza umuhimu wa wanawake kuchangamana na watu mbalimbali hili waweze kujikwamua kiuchumi kuliko kukaa sehemu moja kusubiri fursa ziwafate.
 Mkurugenzi wa Shangwe  Event , Deus Ntukamanzina akizungumza na  Wanawake waliofika katika hafla hiyo na kuwashukuru kwani kukutana kwao ndio mwanzo wa wao kupiga hatua kubwa zaidi
 Mwanasaikolojia na Mshauri wa masuala ya familia , Aunt Sadaka, akieleza umuhimu wa mwanamke kuambatana na mabinti zao katika maisha hili kuwajenga kwa ajili ya kesho yao kuliko kuwaacha nyumbani.
 Meneja mafao kutoka mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF,Rosemary Mchagula akileza umuhimu wa wanawake kujiunga na mfuko huo kutokana na mafao yanayotolewa katika kuwasaidi kwa kulitaja fao la uzazi.
 Balozi wa Wanawake wa Shirika la umoja wa Mataifa nchini(UN),Imelda Lutebinga akichangia mada katika kongamno hilo la Wanawake na maendeleo .
 Afisa Masoko wa Kituo Cha Uwekezaji nchini(TIC), Ratifa Kigoda akileza ni namna gani wanawake wanaweza wakaungana na kuwa wawekezaji wakubw akatika mapinduzi haya ya uchumi wa Viwanda nchini.
 Mmoja ya Wanawake walioshiriki katika kongamano hilo kutoka TIB, Lisa Zavalla akichangia juu ya umuhimu wa wanawake kujikwamjua kiuchumi katika mapinduzi ya uchumi wa Viwanda.
 Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifatilia mada mblimbali zilizokuwa zinaendelea.
 Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifatilia mada mblimbali zilizokuwa zinaendelea.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »