Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, Dkt. Juma Malewa, akisalimiana na Kamishna wa Utawala na Fedha
wa Magereza, Gaston Sanga mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya
Nanenane, Mkoani Mororogoro tayari kwa Kikao Maalum cha Maafisa
Waandamizi wa Jeshi hilo. Kikao hicho kimefanyika kwa siku moja leo 17
Machi, 2018 Mkoani Morogoro.
Kamishna wa Fedha na Utawala wa
Magereza, Gaston Sanga akitoa neno fupi kabla ya kumkaribisha Kamishna
Jenerali wa Magereza kufungua rasmi kikao kazi hicho.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, Dkt. Juma Malewa akiongoza Kikao Maalum cha kujadili mikakati
ya utekelezaji wa Jeshi la Magereza kujitosheleza kwa chakula.
Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini
maelekezo kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa(hayupo pichani).
Washiriki wa Kikao kazi ambao
ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifanya maadiliano
mbalimbali katika vikundi kama inavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Magereza,
Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa
Magereza Mikoa yote Tanzania Bara(waliosimama mstari wa nyuma) mara
baada ya ufunguzi rasmi wa kikao maalum cha kujadili mikakati ya
utekelezaji wa Jeshi la Magereza kujitosheleza kwa chakula. Kikao hicho
kimefanyika kwa siku moja leo 17 Machi, 2018 Mkoani Morogoro
Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza