Waziri Wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akifungua Mkutano Wa
Balaza la Wafanyakazi Wa Wizara ya Afya mapema leo Jijini Dar es salaam.
Mganga Mkuu Wa Serikali Prof.
Muhammad Bakari Kambi akimkaribisha mgeni rasmi Waziri Wa Afya,
Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(hayupo
kwenye picha)
Mkurugenzi Wa Mafunzo na
Rasilimali watu Dkt.Otilie Gowelle wakwanza kulia akifuatilia kwa
makini maagizo ya Waziri Wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu katika mkutano wa
Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Afya uliofanyika jijini Dar es
salaam.
Meza kuu ikiongozwa na Waziri wa
Afya Mhe.Ummy Mwalimu na mganga Mkuu wa Serikali Prof. Kambi wakati
wakiimba wimbo wa kuhamasisha umoja na mshikamano kwa Wafanyakazi, pindi
wakifanya mkutano wa Baraza la Wafanyakazi, Wakwanza ni Katibu wa
Baraza hilo Mary Ntira na wa mwisho ni Afisa Elimu kazi na mratibu wa
Jinsia taifa TUGHE Bw. Nsubisi Mwasandende
Watumishi wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Dorothy Gwajima wapili kutoka kulia.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu katikati waliokaa akiwa
kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi
kutoka Wizara ya Afya mara baada ya kikao cha Baraza hilo kilichofanyika
Leo jijini Dar es salaam.
………………….
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
WATUMISHI wa sekta ya Afya
nchini wametakiwa kujiepusha na vitendo vya kutaka rushwa kutoka kwa
wananchi wanapokuwa sehemu zao za kazi ili kuendana na maadili ya
utumishi wa Umma.
Hayo yamezungumzwa na Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto katika kikao cha
Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es
salaam ili kujadili mustakabari wa utoaji huduma za Afya nchini.
“Marufuku Watumishi wa sekta
ya afya nchini kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa na kama wapo naomba
waache mara moja kwani atakayebainika anajihusisha na rushwa sheria
itafuata mkondo wake mara moja” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
watumishi wa sekta ya afya hasa katika sehemu ya kutolea huduma za afya
wanatakiwa kuwa na lugha nzuri kwa wananchi pindi wanapotoa huduma
sehemu zao za kazi.
Mbali na hayo Waziri Ummy
amewaambia watumishi wa sekta ya afya kuwa kipaumbele katika kutoa elimu
juu ya magonjwa yasioambukiza kwani yamekuwa yakiongezeka kila kukicha
kutokana na ukosefu elimu ya kutosha kuhusu magonjwa hayo.
“Watumishi wa Afya wanatakiwa
kuwa mfano hasa katika kufanya mazoezi, kula lishe bora pamoja na kutoa
elimu ya magonjwa mbalimbali ili kuisaidia kuondoa ongezeko la magonjwa
yasioambukiza” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
ili kufikia adhma ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jonh Pombe Magufuli la kujenga uchumi wa Viwanda ni lazima kuzingatia
utoaji wa huduma bora za afya ili kuwa na wananchi wenye afya ambao
watasukuma gurudumu kufikia lengo hilo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa
Katibu Mkuu Taifa wa Balaza la Wafanya kazi TUGHE Bw. Nsubisi
Mwasandende amesema kuwa katika kutatua changamoto za magonjwa
mbalimbali watendaji wa Wizara ya Afya wanatakiwa kuzingatia hali ya
upatikanaji wa chanjo ili kuboresha huduma za afya.
Aidha Bw. Mwasandende amesema
kuwa watumishi wanatakiwa kulifanyia kazi haraka agizo la Waziri Ummy
Mwalimu la kutokomeza vitendo vya rushwa haraka iwezekanavyo ikiwa kama
moja la adhimio la katiba ya balaza la wafanyakazi.(Chanzo FullshangweBlog)