HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

March 17, 2018

 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa uzinduzi wa Harambee ya kuchangia ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Muheza, kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Masaki Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanaasha Tumbo akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Muheza, kwenye Hoteli.



Na Richard Mwaikenda, Dar

HARAMBEE ya uchangiaji wa ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, umevuka malengo baada ya  wadau kuchangia sh. bilioni 1.6 badala la kadirio la awali la sh. Bil. 1.5.

Jumla ya michango hiyo ilitangazwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa harambee iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Masaki Dar es Salaam jana.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alianza kampeni hiyo ya uchangiaji kwa kutoa sh. milioni 10 na sh. mil. 5 zilizotolewa na wanawe pamoja na wajukuu zake.

AAkizungumza wakati wa uzinduzi huo, Samia alitoa wito kwa wadau wote kuendelea kuchangia kwa manufaa ya nchi na ustawi wa jamii kwa ujumla.

"Niwakumbushe kwa mjenga nchi ni mwananchi,na hivyo ujenzi huu ni hatua kubwa na inayofaa kuungwa mkono na sisi kama Serikali, lakini pia na wadau wote wa maendeleo na wanaoitakia mema Tanzania hii," alisema Makamu wa Rais, Samia na kuongeza...

"Tukizungumzia  Tanzania ya Viwanda tunazungumzia  nguvu kazi; hivyo uwepo wa huduma hizi za afya ni muhimu katika kuhakikisha tuna nguvu kazi yenye afya na siha njema katika kuendesha  viwanda hivi pamoja na kujenga Tanzania mpya inayotarajia kufikia uchumi wa kati siku za karibuni."

Samia aliitaka Tamisemi kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kuratibu upatikanaji wa vifaa, vifaa tiba na watumishi ili huduma stahiki zianze kutolewa mara tu jengo litakapokamilika.

Mama Samia aliupongeza uongozi na wananchi wa Wilaya ya Muheza, kwa kuamua kujenga hospitali hiyo, ili kuboresha hali ya afya na ustawi wa jamii kwa kusogeza huduma za rufaa ngazi ya wilaya karibu na wananchi badala ya kutegemea huduma hiyo kutoka sehemu nyingine na kwamba jambo hilo ni la kupongezwa sana na ni la kuigwa na wengine.

Hivi sasa wananchi wa wilaya hiyo hupata matibabu katika Hospitali ya Kanisa la Kianglikana na Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo iliyo umbali wa Km 72.

Harambee hiyo iliyowashirikisha wadau mbalimbali wapenda maendeleo, iliandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanaasha Tumbo kwa ushirikiano wa uongozi mzima wa wilaya hiyo na mkoa kwa ujumla.

Katika harambee hiyo iliyohanikizwa na Bendi ya Mwanamuziki Mkongwe King Kiki, shairi maalumu na kwaya ya wasanii wa wilaya hiyo pamoja na kuwepo msosi ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Wapo Wadau waliotoa fedha taslimu na wengine kuahidi kutoa fedha, saruji, mabati, mchanga, kokoto, samani, mbao, ujenzi wa barabara pamoja na ujenzi wa baadhi ya wodi, ofisi na mochari.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Tumbo  alisema kuwa kila mwana Muheza ameahidi kuchangia sh. 2,000 na zaidi na baadhi yao wanatumia nguvu zao kusaidia ujenzi wa Hospitali hiyo.

Mhandisi Tumbo, alisema kuwa hospitali hiyo itakayogharimu zaidi ya bil 11 itakapokamilika,imeanza kujengwa kwenye eneo la heka 100 katika Kijiji cha Tanganyika, Kata ya Lusanga, wilayani humo na inatarajiwa kukamilika mwaka 2020.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella, Mbunge wa Jimbo la Muheza, Adadi Rajab, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu, IGP Mstaafu, Said Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu. IMENDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0715264202,0689425467,0754264203




 Baadhi ya wadau wakiwa katika hafla hiyo
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Muheza, Desderia Haule akiwa na baadhi ya wadau
 Mwanamuziki Mkongwe, King Kikii akiwa na  mjumbe wa Kamati ya Harambee hiyo,
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange (katikati), akiwa na Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama wakati wa harambee hiyo. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Mkikita, Neema Ngowi.
 Kwaya ikitumbuiza
 Sehemu ya waalikwa wachangiaji wa harambee hiyo
 Wasanii wakiimba wimbo wa kutoa shukrani kwa Mama Samia kukubali kuwa mgeni rasmi  wa harambee hiyo
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella akitoa pongezi kwa wadau walihudhuria hafla hiyo
 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akielezea mikakati ya kuboresha sekta ya afya nchini ikiwemo ujenzi wa hospitali hiyo ya Wilaya ya Muheza.
 Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo akizungumza katika harambee hiyo ambapo alihakikisha kuunga mkono kwa nguvu zote ujenzi wa hospitali hiyo.

 Mama Samia akibonyeza kitufe kuzindua harambee hiyo
 Shamrashamra za uzinduzi huo
 Mama Samia akifurahia zawadi aliyozawadiwa na uongozi wa wilaya hiyo
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akijaza fomu kuchangia ujenzi wa hospitali hiyo.
 IGP Mstaafu, Said Mwema  akiahidi kuchangia ujenzi wa hospitali hiyo
 Mdau akiahidi kuchangia
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), akipewa mkono wa shukrani na Makamu wa Rais, Mama Samia pamoja na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu baada ya kuahidi kuchangia sh. mil. 1 za kusaidia ujenzi wa hospitali hiyo.
 Rais wa TFF,  Karia akiahidi kuchangia harambee hiyo ambapo aliahidi mapato ya mchezo wa Ngao ya Hisani yataelekezwa kwenye ujenzi wa Hospitali hiyo.
 Wachangiaji wakipongezwa na Viongozi akiwemo Makamu wa Rais, Samia
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ambayo pia kuandaa matamasha ya Pasaka na Chrismas, Alex Msama akipongezwa na Makamu wa Rais, Samia baada ya kuahidi kutoka mchango kufanikisha ujenzi wa hospitali hiyo. Pia aliahidi kutoa mchango kutoka kwenye sehemu ya mapato ya Tamasha la Pasaka.
 Ofisa Uhusiano wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Neema Ngowi akipongezwa na  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kwa kuahidi kutoa sh. mil. 1 zitakazochangwa na wanachama wa matandao huo.
 Msreheshaji wa Harambee hiyo, Charles Mwakipesile akipewa mkono wa shukrani na Makamu wa Rais, Mama Samia baada ya kuahidi kutoa sh. mil 1 za ujenzi wa hospitali hiyo.
 Sasa ni wakati wa msosi

 Viongozi wa Mkikita, CEO Adam Ngamange na  PRO Neema Ngowi wakipata msosi


Makamu wa Rais, Mama Samia akikabidhiwa zawadi ikiwa ni shukrani kwa kufanikisha harambee hiyo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Tumbo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »