Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na
Viongozi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na
Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMUTA) mjini Dodoma.
Akizungumza
baada ya kikao na Makamu wa Rais, Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Khamis
Mkanachi alisema wamekutana na Makamu wa Rais na kumkabidhi ripoti ya
mashindano ya mwaka 2016-2017 na 2017-2018.
Pamoja na
kumkabidhi Ripoti hiyo, pia walimueleza Makamu wa Rais ambaye ni Mlezi wa
Shirikisho, changamoto na mipango mbali mbali ya kuboresha shirikisho hilo. Pichani Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipokea ripoti ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi
na Makampuni Binafsi Tanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirikisho hilo
Bw. Khamis Mkanachi ambaye aliongozana na Uongozi na Wajumbe wa
Shirikisho kukutana na Makamu wa Rais kwenye makazi yake, Kilimani mjini
Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa Shirikisho la Michezo la Mashirika
ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania kwenye makazi yake
Kilimani mjini Dodoma
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Shirikisho la Michezo la
Mashirika ya umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania mara baada ya
kumaliza mazungumzo kwenye makazi yake Kilimani, mjini Dodoma. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)